Ndemla achelewa ndege, ashindwa kuondoka...Soma habari kamili na Matukio360...#share
Na Mwandishi Wetu
KIUNGO mshambuliaji wa Klabu ya
Simba Hamis Ndemla ameshindwa kusafiri kwenda nchini Sweden kwa ajili ya kufanya
majaribio katika klabu ya AFC Eskilstuna kutokana na kukosa ndege ya kuunganisha.
Hamis Ndemla
Taarifa iliyotolewa leo
na Mkuu wa Idara ya Habari na Maewasiliano wa klabu ya Simba Haji Manara
amesema safari hiyo ambayo ilitakiwa kuwa leo imesogezwa mbele.
“Tunapenda
kuwafahamisha kuwa safari ya mchezaji wetu Hamis Said Juma Ndemla iliyokuwa
ifanyike leo Jumanne imesogezwa mbele,” imesema.
Aidha emeeleza kuwa mchezaji huyo ambaye amepata nafasi ya
kwenda kufanya majaribio katika klabu ya AFC Eskilstuna inayoshiriki ligi kuu
nchini Sweden ,sasa ataondoka nchini siku ya Alhamis ya Novemba 9, 2017.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo imebainisha kuwa mabadiliko hayo ya
safari hayataathiri muda wake wa majaribio katika klabu hiyo, ambapo atakuwa
huko kwa siku 14.
Mchezaji huyo alikuwa
akitokea jijini Mbeya na klbu yake ya Simba ambapo mwishoni mwa wiki iliyopita
walikuwa wakicheza na timu ya Mbeya City na katika mcezo huo Simba ilishinda
1-0.
Klabu ya Simba jana ilitangaza kuwa kiungo huyo
amepata nafasi ya kwenda kufanya majaribio nchini Swedeni.
No comments:
Post a Comment