Updates: Polisi wakuta 'vitatu' Ofisini ACT...Soma habari kamili na Matukio360#share
KWA mujibu wa taarifa iliyotolewa na Katibu wa Uenezi, Itikadi
na Mawasiliano ya Umma wa ACT-Wazalendo Ado Shaibu amesema polisi wamekamilisha upekuzi wao katika ofisi za
chama na kutoka na vitu vifuatavyo;
Kiongozi wa Chama cha ACT-Wazalendo Zitto Kabwe
1. Taaarifa ya Kamati ya Uongozi kwa Waandishi wa Habari (Press
Release) ya Tarehe 21 Oktoba 2017 yenye kichwa cha habari "Kamati Kuu ya
ACT Wazalendo Kujadili Hali Mbaya ya Uchumi wa Nchi, Mdororo wa Usalama na
Kuminywa kwa Demokrasia"
2. Taarifa ya Kamati Kuu kwa Waandishi wa Habari (Press Release)
ya Tarehe 28 Oktoba 2017 yenye kichwa cha habari "Ushahidi Kuhusu Kusinyaa
kwa Uchumi wa Nchi Tofauti na Majigambo ya Serikali ya Awamu ya Tano.
3. Vifaa vya Kielektroniki (Laptop na Flash) vilivyotumika
kuandaa taarifa hizo.
Hata hivyo polisi walipofika makao makuu ya chama hicho majira
ya mchana waligoma Kupekuliwa kwa sababu Katibu Mkuu hakuwepo ofisini.
Polisi walifika wakakutana na Katibu wa Uenezi, Itikadi na
Mawasiliano ya Umma, ndugu Ado Shaibu, ambaye baada ya kuwapokea aliwaeleza
kuwa mwenye Ofisi ni Katibu Mkuu ambaye hayuko Ofisini, na kuwa kama Jeshi la
Polisi lilitaka kufanya Upekuzi kwenye Ofisi za ACT Wazalendo, nafasi nzuri
kwao ilikuwa ni jana kwa kuwa walimhoji Katibu Mkuu wa ACT Wazalendo kwa Masaa
7.
Lakini Polisi walisisitiza kufanya upekuzi leo, hivyo wakaamua
kumfuata Katibu Mkuu wa ACT Wazalendo, Dorothy Semu, nyumbani kwake ili awepo
wakati wa upekuzi husika
No comments:
Post a Comment