Ndikumana azikwa Rwanda...soma habari kamili na Matukio360...#share
Na
mwandishi wetu, Rwanda
KOCHA
msaidizi wa Rayon Sports ya Rwanda na aliyekuwa mume wa msanii wa filamu nchini,
Irene Uwoya, mchezaji wa zamani wa timu ya Taifa ya Rwanda na kocha msaidizi wa
Rayon Sport, Ndikumana Hamad Katauti (39) amezikwa jioni ya leo Novemba 15,2017 jijini Kigali, Rwanda.
Ndikumana enzi za uhai wake akiwa na mzazi mwenzake, Irene Uwoya
Hii
leo Daktari mkuu wa timu ya taifa ya Rwanda, Lugemana Charles ameiambia
Matukio360 kuwa amezikwa kutokana na familia yake kutaka hivyo na kwamba sababu
ya kifo chake haijajulikana.
"Ndikumana amezikwa
jioni ya leo kutokana na familia yake kutaka hivyo. Hivyo hatujajua sababu
iliyokatisha uhai wake," amesema
Amesema awali
walipendekeza mwili wa Ndikumana ufanyiwe
uchunguzi lakini familia yake imekataa. "Familia ya Ndikumana ni ya kiislam
hivyo walikataa kufanya uchunguzi kujua sababu ya kifo," amesema daktari huyo
Daktari huyo amesema
hadi juzi jioni walikuwa naye kwenye mazoezi ya timu ya taifa na kwamba
waliachana akiwa mzima.
"Lakini ilipofikia
majira ya saa nne usiku, nilipokea taarifa ya kufariki kwa Ndikumana,
nilishangaa na nikaambiwa kabla hajafa alijisiki vibaya wakampa soda, akatapika
na muda akafariki,’"amesema
Mapema leo taarifa
kutoka Rwanda zilisema Ndikumana Hamad
''Katauti'' ambaye ni mume wa zamani na Baba wa mtoto wa muigizaji maarufu
nchini, Irene Uwoya alifariki dunia usiku wa kuamukia leo bada ya kuugua ghafla.
Kataut alikuwa beki
wa zamani wa Rayon Sports ya Rwanda pia
amewahi kuchezea timu ya soka ya Stand United ya Shinyanga wakati akitokea Cyprus.
Taarifa kutoka
Kigali, Rwanda zinaeleza kwamba alikuwepo
mazoezini jana jioni na hadi anapoteza maisha alikuwa ni kocha msaidizi wa
kikosi cha Rayon Sports ya Rwanda.
Mara ya mwisho alikuja nchini mwaka 2017 wakati wa Simba Day Agosti 8, akitua nchini Agosti 7 akiwa na kikosi cha Rayon ambacho kilicheza na Simba na kupoteza kwa bao 1-0.
No comments:
Post a Comment