NEC yarejesha wagombea tisa udiwani...soma habari kamili na Matukio360..#share
Na mwandishi wetu
TUME ya
Taifa ya Uchaguzi(NEC) imewarejesha wagombea tisa wa kiti cha udiwani waliokuwa
wamewekewa pingamizi na imezikataa rufaa
za wagombea sita.
Mwenyekiti wa NEC, Jaji Semistocles
Kaijage (katikati) akiongoza kikao cha Tume kilichokuwa kinajadili rufaa
za wagombea udiwani pamoja uteuzi wa Wanawake wa udiwani wa viti Maalum.Kushoto
ni Makamu Mwenyekiti Jaji Mkuu Mstaafu (Z) Hamid Mahmoud Hamid na kulia ni
Mkurugenzi wa Uchaguzi ambaye ni Katibu wa Tume, Kailima Ramadhani. (Picha na
NEC).
Hatua hiyo
inafuatia baada ya Novemba 2 na 3, 2017, NEC kupitia rufaa ambapo tisa waliondolewa kugombea, sita waliwekewa pingamizi na wagombea wenzao
lakini pingamizi zao zilikataliwa na msimamizi wa uchaguzi na hivyo kuendelea
kuwepo kwenye orodha ya wagombea na mmoja alipinga kukataliwa kugombea.
Hata hivyo,
Tume baada ya kuchunguza rufaa moja ya mgombea anayepinga kukataliwa kugombea,
imebaini mgombea alikuwa analalamika tu haikuwa rufaa hivyo Nec itamjibu mgombea huyo kwa maadishi malalamiko
yake.
Rufaa
hizo ni mbili ziliwasilishwa na CCM ikipinga walioteuliwa, CHADEMA iliwasilisha
rufaa kumi, saba kati ya hizo ilitaka wagombea wao walioondolewa kwenye orodha
ya wagombea waresheshwe na tatu kilipinga wagombea walioteuliwa.
CUF
iliwasilisha rufaa mmoja ya mgombea wao
ambaye hakuteuliwa, ACT-Wazalendo iliwasilisha rufaa mbili za wagombea wao waliondolewa kugombea kwenye
orodha ya wagombea warejeshwe na UDP iliwasilisha rufaa moja ikipinga mgombea
aliyeteuliwa.
Oktoba
26, 2017 NEC ilipokea taarifa kuwa wagombea 30 kati ya 157 waliorejesha fomu za
uteuzi na kuteuliwa kugombea kwenye
kinyang,anyiro cha uchaguzi mdogo wa marudio wa udiwani katika kata 43
wa Novemba 26, 2017, waliwekewa pingamizi na
wagombea wenzao pamoja na msajili wa vyama vya siasa.
Hata
hivyo, baada ya pingamizi hizo, wasimamizi wa uchaguzi na wasimamizi wasaidizi
ngazi ya kata kwenye maeneo yanayofanya uchaguzi walifanyia maamuzi pingamizi hizo ambapo wagombea
19
waliruhusiwa kuendelea na kampeni za uchaguzi na wagombea 11 waliondolewa
kugombea kwenye nafasi za udiwani.
Sababu
za Msimamizi wa Uchaguzi, Msimamizi Msaidizi wa Uchaguzi, Mgombea na Msajili wa
Vyama vya Siasa kuweka pinganizi ni pamoja na Mgombea kutokuwa raia wa
Tanzania, hajatimiza umri wa miaka 21, hana sifa ya kuwa Mgombea wa Udiwani,
hawezi kusoma na kuandika katika Kiswahili au Kingereza, si mwanachama wa Chama
cha Siasa, si mkazi wa kawaida wa Halmashauri anayogombea.
Sababu
nyingine za Mgombea kuwekewa pingamizi ni kutiwa hatiani kwa kosa la kukwepa
kulipa kodi katika kipindi cha miaka mitano kabla Uchaguzi, kutodhaminiwa na
Wapiga Kura walioandikishwa katika Kata au idadi ya Wapiga Kura inayotakiwa
waliomdhamini haikutimia, kutolipa dhamana ya shilingi elfu tano (5,000/=),
kutokuwa na picha, kutowasilisha Tamko la kisheria, kutodhaminiwa na Chama cha
Siasa kugombea Udiwani.
Zaidi ya hayo, Sababu nyingine za Mgombea kuwekewa pingamizi ni kutotaja gharama na vyanzo vya fedha atakazotumia katika Uchaguzi chini ya Sheria ya Gharama za Uchaguzi ya 2010, kutenda vitendo alivyokatazwa chini ya Sheria ya Gharama ya Uchaguzi, Kutorudisha fomu za uteuzi kwa mujibu wa masharti yaliyowekwa na Sheria, kutotoa Tamko la kuheshimu Maadili ya Uchaguzi ya Mwaka 2015 na kutokuwa na kipato halali kinachomwezesha kuishi.
No comments:
Post a Comment