Conte amtunishia misuli Mourihno...soma habari kamili na Matukio360..#share

Na mwandishi wetu
WAKATI leo timu ya
soka ya Chelsea ikiikaribisha Man United katika uwanja wa Starford Bligde ‘darajani’
kocha Antonie Conte amemwambia Jose Mourihno wa Man United asitarajie ushindi.
Golikipa wa Man United, David Degea akiwa katika harakati za kumkaba Pedro wa Chelsea
Pia Conte amesema Man
City ndio tatizo katika kinyang’anyiro cha kushindana kupata ubingwa wa ligu ya
Uingereza (EPL)
Conte amesema “Sasa kama kuna matatizo makubwa
kwa timu zote ambazo zinapigania kushinda taji la ligi ya Uingereza.Tatizo hilo
ni Manchester City.Iwapo City itaendelea ilivyo itakuwa vigumu kwetu sisi
kuwania taji hilo.lazima tujaribu kufanya vyema lakini si kwa Man United.”
Hata hivyo kocha wa Manchester
United Jose Mourinho amekiri kuwapo kwa tofauti kubwa lakini mwishowe anataka
kumaliza akiwa mshindi kama vile nilivyoshinda akiwa na Inter Milan.
Habari njema ni kwa Chelsea
ambayo inamkaribisha tena kiungo wa kati N'Golo Kante, ambaye amerudi katika
mazoezi baada ya kuwa nje kwa mechi sita na jeraha la nyonga.
Victor Moses
anaendelea kuuguza jereha lakini nahodha Gary Cahill ni sharti aanze baada ya
kukosa kushiriki katika mechi ya ushindi dhidi ya Bournemouth.
Jesse Lingard wa Man
United hatoshiriki mechi hiyo baada ya kutolewa nje katika mechi dhidi ya
Benfica kutokana na tatizo la mgongo.
No comments:
Post a Comment