New Version:Wazazi wahimizeni watoto kupenda masomo sayansi na hesabu...soma habari kamili na Matukio360..#share
Na mwandishi wetu
WAZAZI wametakiwa
kuwatia moyo watoto kupenda masomo ya
sayansi, hesabu na kulipa ada kwa wakati.

Amesema kila mzazi na
mlezi anatakiwa kutobagua watoto katika
mgawanyo wa kazi za nyumbani na pia kutambua wajibu wa kuwafuatilia watoto shuleni hasa maendeleo
ya masomo yanapokuwa hayaendi vizuri.
‘Matokeo ya darasa la
saba ya mwaka 2017, New Version imeng’aa, imeshika nafasi ya pili kiwilaya nafasi
ya tano kimkoa na nafasi ya 96 kitaifa huku ikiwa na wastani wa 205. 1765,’ amesema Mfuko
Shule ya New Version yenye
usajili namba PW.01/7/010 mwaka 2016
katika mtihani wa taifa wa darasa la saba ilishika nafasi ya sita kiwilaya,
nafasi ya 22 kimkoa na nafasi ya 702 kitaifa huku ikiwa na wastani wa 163.0714.
Mwaka 2015 ilishika
nafasi ya kwanza kiwilaya, nafasi ya tano kimkoa na nafasi ya 224 kitaifa huku
ikiwa na wastani wa 201.3913.

Wanafunzi wa darasa la saba katika shule ya msingi New Version iliyopo Kibaha kwa Mathias eneo la Msangani wakiwa wamembeba mmoja wa kijana aliyeongoza katika mtihani wa kitaifa wa darasa la saba, 2017.
Mfuko amesema shule
hiyo inawafundisha watoto kujitambua na kujua wajibu walionao kwa jamii inayowazinguka
na taifa kwa ujumla na kwamba elimu ya mtoto ni
mzazi na mwalimu iwapo kila mtu anatambua wajibu wake na kumthamini mwenzake
kwa nafasi yake.
Maono yao ni kitoa
elimu bora na kujenga jamii yenye
kujitambua ambayo itakuwa ni sehemu muhimu ya kutegemewa na taifa.
Kauli mbiu ya shule hiyo ni
'Education brings self actualization' na mawasiliano yao ni 0712204476 na
0763243650
No comments:
Post a Comment