Mkandarasi apewa miezi miwili kukamilisha barabara...soma habari kamili na Matukio360..#share

Na mwandishi wetu
SERIKALI Mkoani Mbeya imemwagiza mkandarasi wa kampuni ya M/s Chongging Internation Constraction Corporation (CICO) kuwa ifikapo Januari, 2018 kukamilisha mradi wa ujenzi wa barabara   yenye urefu wa kilomita kumi kwa kiwango cha lami  kutoka kijiji cha Lupaso hadi Bujesi.


Mkuu wa mkoa wa Mbeya, Amos Makalla kulia akiwa na mkuu wa wilaya ya Rungwe katikati  akitoa maelekezo kuhusu ujenzi wa barabara kwa kiwango cha lami kutoka kijiji cha Lupaso hadi Bujesi katika halmashauri ya Busekelo.
Mkuu wa mkoa huo, Amos Makalla ametoa agizo hilo leo  katika ziara ya kukagua mradi huo  uliopo katika halmashauri ya Busokelo unaogharimu   bilioni 8.928 zilizotolewa na serikali, lengo  kuboresha miundombinu ili kuharakisha ukuaji wa shughuli  za kiuchumi.

Kaimu meneja wa wakala wa barabara (TANROAD) mkoani Mbeya, mhandisi Eliazary Rweikiza amesema udongo tifutifu unaohifadhi maji muda mrefu ndio changamoto iliyochelewesha ukamilikaji wa mradi huo na imewalazimu kufanya kazi kwa miezi mitatu  tu kwa mwaka.

"Kwa kweli changamoto kubwa ni hiyo kwani eneo hili la mradi utekelezaji wake ni miezi mitatu kwa kila mwaka ambayo  Agosti na Novemba  lakini miezi mingine yote mradi unakwama kutokana na mvua nyingi  zinazonyesha wilayani rungwe," amesema

Mkandarasi wa mradi huo, Wang Cuengbao amesema   utakamilika kwa muda uliopangwa ili kusogeza huduma muhimu za kijamii  na waliingia

mkataba mwaka 2014  na TANROAD .

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search