Nyalandu ashindwa kufanya kampeni...Soma habari kamili na Matukio360

ALIYEKUWA Mbunge wa Singida Kaskazini kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM) Lazaro  Nyalandu ameshidndwa kupanda jukwaani na kampeni za udiwani Mkoani Mtwara.


Lazaro Nyalandu

Mapema leo taarifa kutoka ndani ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) ambapo hivi karibuni alihamia zilibainisha kuwa angeweza kuhutubia katika kampeni za udiwani mkoani humo.

Akithibitisha hilo Mkurugenzi wa Itifaki, Mawasiliano na Mambo ya Nje wa Chadema, John Mrema amesema sababu ni kukosekana kwa ndege ya kuunganisha kutokea Dar es Salaam kwenda Mtwara..

“Kumemsababishia Nyalandu kushindwa kuhudhuria mkutano huo, kwani alikuwa Nairobi nchini Kenya kumjulia hali Tundu Lissu,” amesema Mrema.

Mrema amesema Nyalandu amefika Dar es Salaam na kukosa ndege ya kwenda Mtwara, hivyo amewaomba radhi wananchi ambao walikuwa wanasubiria kumsikiliza Nyalandu na kwamba wanaandaa kwa ajili ya siku nyingine kuweza kufanya hivyo.

"Tunaomba radhi kwa hili ila tukio hilo tunaliandalia mahali pengine na wakati ukifika tutakuwa pamoja naye," amesema Mrema. 

Mwenyekiti wa Chadema Freeman Mbowe jana Jumamosi akihutubia mkutano wa hadhara wa kampeni ya uchaguzi mdogo wa udiwani katika Kata ya Saranga jijini Dar es Salaam alisema amempokea Nyalandu na leo Jumapili Novemba 12, 2017 angeungana naye kwenye mkutano wa kampeni mjini Mtwara.


About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search