Ndovu afanyiwa upasuaji...soma habari kamili na Matukio360...#share
Ndovu huyo anayejulikana kwa jina la Tantor amefanyiwa upasuaji
huo na watu takribani 30 kwa kudungwa
dawa ya kumpa usingizi.
Kwa mujibu wa BBC ni kwamba upasuaji huo ulifanywa kwenye pembe
yake iliyokuwa imepasuka.
Zaidi ya watu 100 walichanga pesa kwa upasuaji huo ambao
uligharimu zaidi ya dola 8,500.
Upasuaji huo ungefanyika miaka miwila iliyopita wakati Tantor
alijeruhi pembe yake, lakini shughuli hiyo ilichelewa baada ya kukosekana kwa
vifaa vinavyostahili ili kufanya upasuaji.
Iibidi vifaa maalumu kutengenezwa kwa upasuaji huo.
Tantor alipekwa katika hifadhi ya Barranquilla Aprili mwaka 1991
wakati alipatwa na shirika la kupambana na madawa ya kulevya nchini Colombia
kwenye shamba moja linalomilikiwa na walanguzi wa madawa ya kulevya.
Anaaminiwa kuwa na umri wa karibu miaka 50.
No comments:
Post a Comment