Polisi wakamata 106 Ubungo...soma habari kamili na Matukio360#...share

Na Salha Mohamed
JESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limekamata watuhumiwa 106 katika kituo kikuu cha mabasi yaendayo mikoani cha Ubungo kutokana na uhalifu.



Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, SACP Lazaro Mambosasa

Akizunguma leo  jijini Dar es Salaam  Kamanda wa Polisi Kanda hiyo,  SACP Lazaro Mambosasa  
amesema Polisi walifanya operesheni kali leo alfajiri katika kituo hicho kufuatia ongezeko la wimbi la uhalifu unaofanyika kwa abiria na mali zao.

"Operesheni hiyo imefanikisha kukamata watuhumiwa 106 ambapo watuhumiwa 95 walikamatwa kwa makosa ya kubughudhi abiria, kuibia abiria, kuuza tiketi zisizo halali (bandia) na kujivalisha sare za mawakala wa mabasi ili hali wao si mawakala wa mabasi husika," amesema.

Amesema watuhumiwa  wote wamefikishwa katika mahakama ya jiji.

Amesema baada ya uchambuzi  watuhumiwa 11 walibainika kuwa na kesi mbalimbali zinazoendelea ambapo wamepelekwa kituo kikuu cha magomeni ili kuendelea na tuhuma zinazowakabili.

Mambosasa amewataja watuhumiwa hao kuwa ni Ahmed Said(21) mkazi wa Ubungo,Suleiman Abdallah(30)  mkazi wa Kinana, Ally Shango(20)
mkazi wa Kinana.

Wengine ni Yusuph Okocha(25)mkazi wa Mabibo,Idd Mohamed (22) mkazi wa Ubungo, Yusuph Chuma(22)Mkazi wa Manzese.

"Wengine ni Baraka Makunda (31)mkazi wa Temeke, JUMA Bakabibi (38) mkazi wa Buguruni, JUMA Badoni (22) mkazi wa Ubungo, Saladini Abdul (30)
mkazi wa Ubungo na Rashid Juma(17) mkazi wa Ubungo.


"Msako huu utakuwa endelevu katika stendi za Mbezi, Temeke na vituo vyote vya mabasi ya abiria na mizigo, "amesema. 

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search