Serikali iwawezeshe maofisa ugani...soma habari kamili na Matukio360...#share
SERIKALI imetakiwa kuwawezesha kifedha Maofisa Ugani wa kilimo na
ufugaji ili waweza kuwafikia wakulima wengi kwa urahisi.
Mkurugenzi wa Jukwaa Huru la Wadau wa Kilimo (ANSAF) Audax Rukonge, akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam.
Hayo yamesemwa leo jijini Dar es Salaam na Mhadhiri wa Chuo
Kikuu cha Kilimo Cha Sokoine (SUA) Dk. Sizya Lugeye akizungumza na waandishi wahabari
katika Mkutano wa Jukwaa Huru la Wadau wa Kilimo (ANSAF) ulioshirikisha wadau mbali
mbali wakilimo na ufugaji, ameseam Maofisa Ugani wengi hawana nyenzo za kuwafikia wakulima.
“Hawajeweza kuwafikia wakulima wengi, kwa sababu nyenzo nyingi
hawana, wanaishi bila baiskeli, pikipiki kwa hiyo wapo pale katika ngazi za vijiji,
kata na wengine ngazi ya wilaya lakini hawatoki na hawajui kinachoendelea katika
ngazi za chini yao,” amesema Dk. Lugeye.
Aidha ameitaka serikali kufikilia kubadili sera ya kuwa na Ofisa
Ugani kila wilaya na badala yake kuwe na wataalamu wa ugani katika ngazi ya kata
ambao wamewezeshwa kwa kupewa nyenzo zote zinazohitajika ili waweze kuwa watendaji
wazuri.
Ameongeza kuwa serikali iongeze bajeti katika sekta ya kilimo
na igawanywe katika kila wilaya.
Kwaupande wake Mkurugenzi wa ANSAF Audax Rukonge, akizungumza juu
ya mkutano huo, amesema wamekutana kwa ajili ya kujadiliana kuhusu jinsi ya utoaji
wa huduma za ugani kwa ubora unaostahili, ili kuendana na mbio za kuongeza tija
katika uzalishaji na upatikanaji wa chakula hususani katika kipindi hiki nchi inapolenga
kuwa ya viwanda.
Amesema kuwa wakulima wamekuwa wakilalamikia kuhusu ubora wa huduma
kutoka kwa wagani, hivyo watatumia mkutano huo kujadili jinsi bora ya kuweza kuboresha
huduma hizo ili kumsaidia mkulima kuzalisha zaidi lakini mazao yaliyo bora.
Amesema hilo litawasaidia wakulima kupata soko la ndani na katika
ukanda wa Afrika Mashariki.
Aidhaa mesema kuna haja ya kubadili mfumo wautoaji wahuduma za
ugani kwa wakulima kwa kuweza kuweka rasilimali zakutosha katika vituo vya utoaji
wahuduma hizo pamoja na kutoa elimu kwa Maofisa Ugani.
Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Kilimo Cha Sokoine (SUA) Dk. Sizya Lugeye akizungumza na waandishi wahabari jiji Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment