TECNO, VODACOM kuitambulisha PHANTOM 8...soma habari kamili na Matukio360..#share
Mkuu kitengo cha mahusiano Vodacom Jackline
Phantom 8 ina 6GB RAM,Betri yake ina uimara wa 3500 mAh za kuhifadhi chaji kwa muda mrefu, 64 GB ROM, inayoipa simu uwezo wa ziada wa kuhifadhi data kufikia 2TB , Inavuta picha iliyombali kwa ukaribu bila kupoteza muonekano halisi mara 10 zaidi ya simu za kawaida . Phantom 8 ina muundo na mtindo wa kuvutia hasa rangi yake yenye mng’ao wa almasi

Kampuni kinara ya simu za mkononi TECNO imeungana na Vodacom kutambulisha toleo jipya TECNO Phantom 8, Simu hiyo iliyozinduliwa nchini Dubai imetambulishwa rasmi nchini Tanzania katika duka la TECNO SMART HUB lililopo Mlimani City mapema mwezi huu.
Akizungumza wakati wa utambulisho , Afisa mahusiano wa TECNO , Eric Mkomoya amesema ‘’ TECNO tumeitambulisha rasmi Phantom 8 nchini Tanzania leo tukiwa na mshirika wetu wa matoleo ya Phantom nchini , Vodacom .Tumetengeneza simu bora yenye hadhi, tunayofuraha kuwataarifu wateja wetu kuwa Phantom 8 inapatikana katika Smart Hubs za TECNO na maduka yote ya Vodacom nchini.’’ Alihitimisha
Akizungumza na waandishi wa habari Mkuu kitengo cha mahusiano Vodacom Jackline amesema ‘’ TECNO inataraji wateja wake kufurahia matumizi ya toleo jipya la simu janja iliyopo sokoni ambayo tayari imejipatia umaarufu kwa kupokelewa vizuri sehemu mbali mbali nchini Tanzania. Vodacom inawazawadia meseji 300 , 5GB za kuperuzi mtandaoni , na dakika 300 za kupiga mitandao yote kwa wateja watakao nunua Phantom 8 katika maduka ya Vodacom yaliyopo nchini kote nchini
Ushirikiano baina ya TECNO na Vodacom umekua wa kudumu ambapo awali waliitambulisha Phantom 6 na 6+ sasa wanakuletea Phantom 8 inayotikisa soko ikiwa na 20MP kamera ya mbele na 12MP +13 MP kamera zake 2 za nyuma.
Mwandishi wa habari Asia Matona alijinyakulia zawadi ya Phantom 8 kwa hisani ya TECNO na Vodacom.
No comments:
Post a Comment