Serikali kupima upya mashamba ya ushirika...soma habari kamili na Matukio360...#share
Na mwandishi wetu
SERIKALI ipo katika mkakati wa kuandaa na kupima upya
mashamba ya vyama vya ushirika mkoani Kilimanjaro
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi aliyesimama akizungumza na watendaji.
Kauli hiyo imetolewa leo Bungeni mjini Dodoma na waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendele ya Makazi, William
Lukuvi alipokuwa akijibu swali la mbunge kuhusu mpango wa serikali wa mashamba
ya ushirika mkoani Kilimanjaro
“Pamoja na
mambo mengine Serikali inaanda utaratibu wa upimaji upya mashamba yote ya
ushirika mkoani Kilimanjaro,” amesema Lukuvi
Amesema tayari ameshaiandikia wizara ya kilimo na pia
kukutana kimazungumzo na wahusika wa wizara hiyo kwa kuwa mashamba hayo yapo
chini yao.
Lukuvi amesema mchakato ukimalizika uenda mashamba
hayo yakagawiwa kwa wananchi kadri inavyofaa ili kuyaendeleza.
No comments:
Post a Comment