Serikali kupunguza mimba za utotoni...Soma habari kamili na Matukio360...#share

Na Abraham Ntambara

SERIKALI  imejipanga kupunguza mimba za utotoni  kwa asilimia 27 kwa kipindi cha  miaka mitano kinachoanzia  2017 hadi 2022 lengo likiwa ni kuhakikisha mtoto wa kike anapata haki yake ya elimu.
Mkurugenzi Mtendaji wa Jukwaa la Utu wa Mtoto wa Kike (CDF) Koshuma Mtengeti, akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam

Hayo yamesema leo Jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi wa Maendeleo ya watoto kutoka Wizara ya Afya ,Maendeleo ya Jamii Jinsia, Wazee na Watoto, Margaret Mussai wakati wa Kongamano la Mtoto wa Kike , liloandaliwa na Jukwaa la  Utu wa Mtoto wa Kike (CDF) kwa udhamini wa Shirika la Maendeleo  Uswidi ( Swedish International Development Cooperative Agency-SIDA).

Mussai amesema kwa sasa serikali imeandaa mpango kazi wa Taifa wa kotokomeza ukatili wa kijinsi kwa upande  Mimba za Utoto.

“Katika Mpango  huu tumeanza kupunguza mimba kwa asilimia 27 kwa watoto na tunaamini mpango huu utasaidia kundokana na tatizo hili”amesema

Amesema katika kutekeleza mpango huu, Serikali  itashirikiana Taasisi zisizo za Kiserikali  katika kuhakikisha wanapunguza Mimba za Watoto.

Hata hivyo , Mussai amewataka Watoto wa Kike  kujitambua wenyewe kwa kujiepesha na mambo yasio faa ambayo yatapelekea kuongezeka mimba za watoto ambapo amedai zimechangiwa na watoto hao kujiingiza kwenye makundi yasioa faa.

Kw upande wake Mkurugenzi wa Mtendaji wa CDF Koshuma Mtengeti, amesema lengo la kongamano hilo ni kuwapatia fursa watoto wa kike kukurana na Mkurugenzi Mwandamizi wa Shirika la Uswid  ambapo watapata fursa ya kuelezea mafunzo mbali mbali waliyopata kutokana na utekelezaji wa miradi mbali mbali ya CDF.

Amesema miradi hiyo ni pamoja na miradi ya kutokomeza, mimba za utotoni, ndoa za utotoni, ukatili wa kijinsia na kuonesha kazi za ujasiriamali walizozifanya ikiwa kama mafanikio ya miradi ya CDF.

“Vile vile katika kongamano hili, wanaume na wavulana wakiwa kama mabalozi wa CDF watapata fursa ya kuelezea ni kwa namna gani wanafanya kazi za kuelimisha jamii pamoja na vijana rika juu ya madhara ya ukatili wa kijinsia, ukeketaji, mimba za utotoni pamoja na ndoa za utotoni ili kufikia dhana ya Taifa ya kuleta usawa wa kiiinsia,” amesema Mtengeti.

Naye Mkurugenzi Mwandamizi kutoka SIDA Carin Jamtin, amesema shirika lao limekuwa likitetea haki za woto kwa kuhakikisha watoto wakike na kiume wanakuwa na haki sawa katika jamii hususani haki ya kupata elimu.


Mkurugenzi Mwandamizi wa Shirika la Maendeleo  Uswidi ( Swedish International Development Cooperative Agency-SIDA) Carin Jamtin, akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam.


Mkurugenzi wa Maendeleo ya watoto kutoka Wizara ya Afya ,Maendeleo ya Jamii jinsia na Watoto, Margaret Mussai, akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam.


About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search