'Updates' Kupekuliwa ofisi ACT Wazalendo...Soma habari kamili na Matukio360... #share

Kuhusu Kupekuliwa kwa  Ofisi ya Makao Makuu ya ACT Wazalendo
h
Kiongozi wa Chama cha ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe.
1. Leo tarehe 9 Oktoba 2017, Kaimu Katibu Mkuu wa ACT Wazalendo Ndugu Dorothy Semu aliitikia wito wa jeshi la Polisi (Kituo cha Makosa ya Kifedha, Kamata, Dar es salaam) waliomtaka kwenda kutoa maelezo ya ziada kuhusu nyaraka na vifaa vya kieletroniki vilivyochukuliwa kwenye Ofisi za Makao Makuu ya ACT Wazalendo

2. Ikumbukwe kuwa juzi tarehe 7 Novemba 2017 Jeshi la Polisi lilifanya upekuzi katika Makao Makuu ya ACT Wazalendo yaliyopo Kijitonyama Jijini Dar es salaam na kuondoka na nyaraka za chama kuhusu Kusinyaa kwa uchumi wa nchi na vifaa vya kielektroniki (flash na laptop) vilivyotumika kuandaa taarifa hizo za kiuchambuzi.

3. Ni zaidi ya wiki sasa tangu Kiongozi wa Chama Ndugu Zitto Kabwe aitwe na Jeshi la Polisi kwanza kwa tuhuma za uchochezi kisha uchambuzi wa Kamati Kuu kuhusu Kusinyaa kwa uchumi. Tangu kuitwa kwake kwa mara ya kwanza tarehe 31 Oktoba 2017 katika siku zilizofuatia yeye mwenyewe na viongozi wengine kadhaa wa Chama wameitwa kuhojiwa na Jeshi la Polisi.

4. Kama tulivyoeleza huko awali, danadana hizi za Jeshi la polisi zimeathiri kwa sehemu kubwa ushiriki wetu kwenye Kampeni za marudio ya uchaguzi wa madiwani. Hivyo basi, kuanzia sasa, viongozi wetu watatawanyika mikoani kuendelea na kampeni. Kama jeshi la polisi litataka kuwahoji viongozi wetu litapaswa kutengeneza utaratibu ambao hauathiri ushiriki wetu wa Kampeni. Kwa kuanzia, Kaimu Mwenyekiti wa Chama Ndugu Yeremia Kulwa Maganja atafanya ziara kwenye mikoa ya Ruvuma, Lindi na Mtwara kushiriki ufunguzi wa Kampeni kwenye kata zilizopo kwenye mikoa hiyo ambazo zinarudia uchaguzi.

Ado Shaibu,
Katibu wa Itikadi, Mawasiliano na Uenezi,
ACT Wazalendo
Imetolewa Leo tarehe 09 Novemba 2017

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search