Serikali yapata sh. bilioni 1.6 mrahaba madini ya Almasi...Soma habari kamili na Matukio360...#share
Abraham Ntambara
SERIKALI imepata sh. Bilioni 1.614 kutokana na mauzo kwa njia
ya mnada wa madini ya almasi ya Kampuni ya Williamson Diamonds Ltd.
Waziri wa Madini Angela Kairuki akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam.
Madini hayo ni kiasi cha karati 39,567.96 kilichozalishwa na
Kampuni hiyo kwa ruhusa ya serikali na kuomba wauze.
Serikali ilikubali na wataalamu wa serikali walithaminisha
almasi hizo na kupata thamani ya awali ya Dola za Marekani 8,191,644.99 na
mrahaba wa awali ukalipwa Dola za Marekani 491,498.70 na ada ya ukaguzi Dola za
Marekani 81,916.45 na hivyo serikali kupata Dola za Marekani 573,418.15 sawa na
sh.bilioni 1.288.
Akizungumza leo na waandishi wa habari jijini Dar es Slaam
Waziri wa Madini, Angela Kairuki, amesema madini hayo yalisafirishwa Oktoba 20,
2017 kwenda nchini Ubelgiji na kuuzwa jana chini ya usimamizi wa maofisa wa
Serikali.
“Oktoba 20,2017 almasi hizo zilisafirishwa kwenda Ubelgiji na
serikali ilituma maofisa wake kusimamia uuzwaji wa almasi hizo, ziliuzwa kwa
njia ya mnada jana, almasi hizo zilikuwa kwa Dola za Marekani 10,261,227.76.
Thamani hii ni sawa na asilimia 20.16 kulingana na thamani ya usaminishaji wa
awali,” amesema Kairuki.
Amesema kutokana na ongezeko hilo baada ya almasi hizo
kuuzwa, serikali itapata mrahaba zaidi ambao ni wa mwisho (Final royalty) kiasi
cha Dola za Marekani 124,174.97 na ada ya ukaguzi Dola za Marekani 20,695.83
ambayo jumla yake ni Dola za Marekani 144,870.80 sawa n ash. Milioni 325.525.
Hivyo amesema jumla ya mapato yote kutokana na mauzo hayo ni
Dola za Kimarekani 718,288.95.
Aidha amesema baada ya serikali kuzuia mzigo wa almasi wa
kampuni hiyo zilizokuwa zisafirishwe Antwerp-Ubelgiji Agosti 31, 2017 ili
kujiridhisha kuhusu thamani halisi ya
almasi hizo bado upo na taratibu za
kuthibitisha thamani halisi zinaendelea.
Katika hatua nyingine Waziri Kairuki amesema usiku wa kuamkia
Oktoba 29, 2017 katika eneo la Kiabakari, serikali ilikamata sampuli za miamba ya madini ya dhahabu
takribani kilo 600 zilizokuwa zinasafirishwa na Kampuni ya wachina inayoitwa
ZEM (T) Ltd bila vibari kutoka wizara ya madini.
Hivyo serikali imeamua kuwapeleka mahakamani ili sharia
ichukue mkondo wake.
No comments:
Post a Comment