NBS: Mfumuko wa bei washuka...Soma habari kamili na Matukio360...#share
Na Abraham Ntambara
MFUMUKO wa bei nchini kwa mwezi Oktoba, 2017 umeshuka hadi
kufikia asilimia 5.1 ikilinganishwa na asilimia 5.3 ilivyokuwa mwezi Septemba,
2017.
Mkurugenzi wa Shughuli za Kitakwimu, Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) Irenius Ruyobya, akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam.
Hayo yamebainishwa leo jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi wa
Shughuli za Kitakwimu kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu, Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS)
Irenius Ruyobya, amesema hiyo inamanisha kuwa, kasi ya mabadiliko ya bei za
bidhaa na huduma kwa mwaka ulioishia mwezi Oktoba, 2017 imepungua
ikilinganishwa na kasi ya ilivyokuwa kwa mwaka ulioishia mwezi Septemba, 2017.
Aidha amesema kushuka kwa Mfumuko wa Bei wa mwezi Oktoba,
2017 kumechangiwa na kushuka kwa bei za bidhaa ya baadhi za vyakula kwa kipindi
kilichoishia mwezi Oktoba, 2017 zikilinganishwa na bei za mwezi Oktoba 2016.
“Baadhi ya bidhaa za vyakuli zilizochangia kupungua kwa Mfumuko
wa Bei ni pamoja na, unga wa mtama kwa asilimia 2.6, samaki kwa asilimia 7.1,
matunda kwa asilimia 2.7, mbogamboga kwa asilimia 7.4, maharage kwa asilimia
2.9,viazi kwa asilimia 14.4, na karanga kwa asilimia 7.8,” amesema Ruyobya.
Ruyobya ameongeza kuwa
Mfumuko wa Bei nchini una mwelekeo unaofanana na baadhi ya nchi nyingine za
Afrika Mashariki ambapo nchini Kenya Mfumuko wa Bei wa mwezi Oktoba, 2017
umeshuka hadi asilimia 5.72 kutoka asilimia 7.06 mwezi Septemba, 2017 na nchini
Uganda umeshuka hadi asilimia 4.8 mwezi Oktoba, 2017 kutoka asilimia 5.3 mwezi
Septemba, 2017.
No comments:
Post a Comment