Serikali yasajili machapisho 109...Soma habari kamili na Matukio360../#share
Na Mwandishi Wetu
SERIKALI imesema hadi kufikia Oktoba 31, 2017, ambayo ni siku ya mwisho ya utoaji wa leseni kwa machapisho ya zamani, Idara imetoa leseni za machapisho 109 na kati ya hayo 85 ya zamani na 24 mapya.
Mkurugenzi Mkuu, Idara ya Habari -Maelezo na Msemaji Mkuu wa Serikali Dk. Hassan Abbasi.
Aidha imepiga marufuku kuanzia sasa kutoa machapisho ya magazeti na vijarida kwa watu binafsi na taasisi ambazo hazikukamilisha taratibu za usajili na kupatiwa leseni kwa muda uliokuwa umewekwa.
Aidha imepiga marufuku kuanzia sasa kutoa machapisho ya magazeti na vijarida kwa watu binafsi na taasisi ambazo hazikukamilisha taratibu za usajili na kupatiwa leseni kwa muda uliokuwa umewekwa.
Taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari leo na Mkurugenzi Mkuu, Idara ya Habari -Maelezo na Msemaji Mkuu wa Serikali Dk. Hassan Abbasi, imesema kuwa utoaji wa leseni kwa machapisho yaliyosajiliwa nchini ni utekelezaji wa matakwa ya kifungu cha 5(e) cha sheria hiyo.
“Serikali kupitia Idara ya Habari (Maelezo) inautaarifu umma
kuwa juzi , oktoba 31, 2017, imekamilisha awamu ya kwanza ya utoaji wa leseni
za uchapishaji wa magazeti na majarida yaliyokuwa yamesajiliwa awali kabla ya
kuanza kutumika kwa sheria mpya ya Huduma za Habari No. 12 ya mwaka 2016 na
kanuni zake za mwaka 2017,” imesema.
Aidha imesema baada ya kumalizika kwa kipindi hicho ambacho
kilikuwa ni muda wa nyongeza baada ya agizo la awali kumalizika Oktoba 15 mawa
huu, omeeleza kuwa watu binafsi na taaasisi ambazo hazikukamilisha taratibu
husika ndani ya kipindi hicho kuwa kwa sasa hawataruhusiwa tena kuendelea kutoa
machapisho hayo hadi watakapo pata leseni Mpahya.
Mbali na hilo, imesema kuwa ni muhimu kufahamu kuwa ni kosa
la jinai kuchapisha gazeti, jarida au machapisho mengine yaliyoainishwa kwa
mujibu wa sheria bila kuwa na leseni, isipokuwa kwa idhini maalumu tu, kwani
kwa mujibu wa kifungu cha 50(2) (a) cha Sheria ya Huduma za Habari, 2016,
ikithibitika kutendeka kosa hilo adhabu ni faini kati ya sh. Milioni 5 hadi 10,
kifungo cha miaka mitatu hadi mitano au vyote kwa pamoja.
Aidha idara imesema itaendelea kutoa huduma za kutoa leseni
mpya kwa machapisho ya zamani na mapya.
Agosti 23, 2017 serikali ilitangaza kufanya usajili mpya na utoaji wa leseni kwa magazeti na vijarida ambapo ilitoa muda wakukamilisha zoezi hilo kuwa Oktoba 15, lakini baadaye muda huo uliongezwa hadi Oktoba 31, 2017.
Taarifa ya Serikali
No comments:
Post a Comment