Simba yamruhusu Ndemla kwenda Sweden....soma habari kamili na Matukio360..#share
Na mwandishi wetu
KIUNGO mshambuliaji wa Klabu ya Simba Hamis Ndemla amepata nafasi ya kwenda kufanya majaribio katika klabu ya AFC Eskilstuma inayoshiriki ligi kuu nchini Sweeden.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa kwa umma na mkuu wa Kitengo cha Habari wa klabu hiyo, Haji Manara imesema Ndemla anatarajiwa kuondoka nchini kesho Novemba 7, 2017. Atakuwa kwenye majaribio kwa siku 14 nchini humo.
"Klabu ya Simba inayofuraha kutangaza kuwa mchezaji wake Hamis Said Juma (Ndemla) amepata nafasi ya kwenda kufanya majaribio ya kucheza soka la kulipwa nchini Sweeden.
No comments:
Post a Comment