Kiungo Mbeya City apanga kuinyoosha Yanga...Soma habari kamili na Matukio360..#share
NA MWANDISHI WETU
KIUNGO mshambuliaji wa Mbeya City,Mohamed Mkopi,
ameapa kuiua Yanga kama atapata nafasi ya kucheza pambano kati ya timu hizo
ambao umepangwa kupigwa kwenye Uwanja wa Uhuru,Dar es Salaam.
Kikosi cha Timu ya Mbeya City
Mkopi amefanikiwa kuifungia Mbeya City bao moja katika Ligi Kuu
Tanzania Bara inayoendelea sambamba na kutoa pasi tano zilizowezesha kupatikana
kwa mabao.
Mohamed amesema ameifatilia a Yanga kwenye michezo yake zaidi ya
mmoja na kubaini mapungufu yao ambayo anaamini atayatumia
kuwafunga kama atapata nafasi yankucheza mchezo kati ya timu hizo.
“Siwezi kuwabeza kwani wana timu nzuri yenye wachezaji
wazuri ambao wanabadirika kutokana na aina ya mchezo, lakini kama
nitapata nafasi ya kucheza hawataweza kunizuia kutimiza lengo langu,” amesema.
Amesema kuwa msimu huu amepania kurudi katika ubora wake mara
baada ya uliopita kuwa nje ya uwanja baada ya kufungiwa na Shirikisho la
Soka Tanzania(TFF )kutokana na usajili wake kukiuka taratibu.
No comments:
Post a Comment