SUMATRA : Disemba mwisho kuzungumza siasa, dini, biashara ndani ya basi
Na
mwandishi wetu
MAMLAKA ya usimamizi wa usafri wa nchi kavu na majini (SUMATRA) inatarajia kuwa Disemba,
2017 itakuwa mwisho kwa abiria kuzungumza masuala ya siasa, dini na kufanya
biashara wawapo safarini.
Mkurugenzi Mkuu Mamlaka ya Udhibiti Usafiri wa Nchi Kavu na Majini(SUMATRA),Gilliard Ngewe
Agizo
hilo limezidi kusisitizwa leo na ofisa
elimu wa Sumatra, Nicolas Kinyelili na kwamba kanuni ya leseni ikikamilika
zoezi hilo litaanza mara moja.
"Duniani
kote hakuna mahala watu wanapomaliza uchaguzi wanaendelea na siasa, mambo ya
mazungumzo ya dini yanamahala pake na hata biashara," amesema Kinyelili
Amesema
kanuni mpya za leseni ya usafirishaji zinakaribia kukamilika na zimezingatia
matakwa na taratibu za usafirishaji. " Uenda Disemba, 2017 zikaanza kazi.'' amesema
Hivi
karibuni mkurugenzi mkuu wa Sumatra, Gilliard Ngewe amenukuliwa akisema dereva
na abiria atakayebainika kufanya vitendo hivyo hatua kali za kisheria
zitachukuliwa dhidi yake na kwa wasafirishaji watanyanganywa leseni.
Agizo
hilo linakuja baada ya hivi karibuni kudaiwa kuwapo kwa mvutano wa kupinga
kanuni mpya kati ya Sumatra na chama cha wamiliki mabasi yaendayo mikoani
(Taboa) na wa usafiri Dar es Salaam
(UWAMADAR)
Taboa
na Uwamadar wamedai kuwapo katika malumbano na Sumatra kuhusu kanuni hizo mpya zinazotarajia kutumika hivi karibuni baada ya
mchakato wake kukamilika.
Mkurugenzi
wa huduma za sheria wa Sumatra, Tumaini Silaa amesema Sumatra ipo kwa ajili ya
kuhakikisha wadau wote wa usafiri wanapata haki sawa.
Amesema
kanuni mpya bado zipo katika mchakato na kwamba haziwezi kuanza hadi hapo wadau
wote watakapokubaliana.
‘Kimsingi
mambo haya ya kanuni mpya haziwezi
kuanza kabla ya kujadiliana na wadau wote wa usafiri, hivyo naamini hili
haliwezi kuwa jambo kubwa sana na litapatiwa mfumbuzi,’ amesema.
No comments:
Post a Comment