Kesi dawa za kulevya Masogange kuanza kujitetea..soma habari kamili na Matukio360..#share
Na
Abdulrahim Sadiki
JANUARI
17, 2018 Agnes Gerald ‘Masogange’ ataanza kujitetea dhidi ya shtaka la kutumia
dawa za kulevya linalomkabili katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.
Mnogeshaji, Agnes Gerald 'Masogange'
Mshtakiwa
huyo ambaye ni mnogeshaji wa video (Video Qeen),alipaswa kuanza kujitetea leo kwa Hakimu Mkazi Mkuu, Wilbard Mashauri lakini imeshindikana kwa sababu hajaandaliwa.
Wakili
Nehemia Nkoko ameeleza kuwa kesi ilipangwa kwa ajili ya Masogange kuanza
kujitetea lakini hawakumuandaa kutokana na kupata msiba
Hakimu
alikubaliana na hoja hiyo na kuiahirisha hadi Januari 17,2018 atakapoanza
kujitetea.
Hatua
hiyo imefikiwa mara baada ya Hakimu Mashauri kumuona mshtakiwa huyo kuwa ana
kesi ya kujibu na kwamba anapaswa kujitetea na kuwaita mashahidi wa kumsaidia
ambapo anatarajia kuwaita mashahidi watatu.
Masogane
anatetewa na Mawakili Nehemia Nkoko na
Ruben Simwanza. Kesi
hiyo inaendeshwa na Wakili wa Serikali,
Costantine Kakula ambaye kwa upande wao
waliwaita mashahidi watatu wa upande wa mashtaka kutoa ushahidi wao na
kuufunga.
Masogange
anakabiliwa na mashtaka mawili
ya kutumia dawa za kulevya aina ya Heroin na Oxazepam.
Anadaiwa
kufanya makosa hayo chini ya kifungu cha 18 (a) cha sheria ya kupambana na dawa
za kulevya namba 5 ya mwaka 2015.
Katika kesi hiyo
namba 77 ya mwaka 2017,
Masogange anadaiwa
kuwa kati ya Februari 7 na 14,2017 katika maeneo yasiyojulikana ndani ya jiji
la Dar es Salaam alitumia dawa za
kulevya aina ya Heroin (Diacety Imophine).
Pia anadaiwa kuwa
kati ya Februari 7 na 14,2017 alitumia
dawa za kulevya aina ya Oxazepam.
No comments:
Post a Comment