Sumatra, Taboa wakanusha mgomo, wakili kulumbana ...soma habari kamili na Matukio360..#share
Na
Abraham Ntambara
MAMLAKA
YA Usimamizi wa usafri wa nchi kavu na majini (SUMATRA) na Chama cha wamiliki
mabasi yaendayo mikoani (Taboa) wamekanusha kuwapo kwa mgomo wa
usafirishaji unaoelezwa kuwapo kuanzia
kesho.
Wadau wa Usafirishaji, kutoka kulia ni Issa Nkya Mweka Hazina Taboa, Kismat Dhalla Mwenyekiti UWADAR, Tumaini Silaa Mkurugenzi wa Huduma za Sheria Sumatra wakizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam.
Pia
wamekili kulumbana katika kanuni na sheria mpya zinazotarajia kutumika hivi
karibuni baada ya mchakato wake kukamilika.
Leo
jijini Dar es Salaam Mwenyekiti wa wadau wa usafirishaji UWADAR, Kismat Dhalla
amekanusha taarifa zilizozagaa kwenye mitandao kuwapo kwa mgomo huo na kwamba
taarifa hizo ni uongo
‘Hakuna
mgomo wowote uliotangazwa na wasafirishaji(Taboa) hivyo wadau wa usafirishaji waendelee na
shughuli zao kama kawaida,’ amesema Dhalla.
Dhalla
amesema pamoja na mambo mengine Jumatano wiki watakaa na Sumatra kujadili
masuala kadhaa ikiwamo kanuni na sheria mpya za usafirishaji.
Mweka
hazina wa Taboa, Issa Nkya amesema wapo kwenye msuguano na Sumatra kuhusu
kanuni na sheria hizo na kwamba watazipatia ufumbuzi muda si mrefu.
Mkurugenzi
wa huduma za sheria wa Sumatra, Tumaini Silaa amesema Sumatra ipo kwa ajili ya
kuhakikisha wadau wote wa usafiri wanapata haki sawa.
Amesema
sheria na kanuni mpya bado zipo katika mchakato na kwamba haziwezi kuanza hadi
hapo wadau wote watakapokubaliana.
‘Kimsingi
mambo haya ya kisheria na kanuni mpya haziwezi kuanza kabla ya kujadiliana na
wadau wote wa usafiri, hivyo naamini hili haliwezi kuwa jambo kubwa sana na
litapatiwa mfumbuzi,’ amesema.
No comments:
Post a Comment