'UPDATES' Kifo Kanumba, Lulu miaka miwili jela...Soma habari kamili na Matukio360...#share
Na Abdulrahim Sadiki
LEO Novemba 13, 2017 Mahakama Kuu ya Tanzania imemtia hatiani kuua bila kukusudia na kumhukumu miaka miwili jela msanii wa filamu, Elizabeth Michael 'Lulu'.
Masnii wa filamu, Elizabeth Michael 'Lulu'
Hatua hiyo imefuatia baada ya wazee watatu wa Baraza kutoa ushauri wao kwa mahakama kwamba Lulu' ameua bila kukusudia au la.
Lulu alikabiliwa na kesi ya kuuwa bila kukusudia, akidaiwa kumuuwa msanii mwenzake, Steven Kanumba April 7, 2012.
Awali kabla ya wazee kutoa maoni hayo, Jaji Sam Rumanyika alisoma maelezo ya ushahidi wa pande zote mbili kisha kusikiliza maoni hayo.
Kabla ya kutoa maoni hayo, Jaji Rumanyika alisema kimsingi ushahidi wa upande wa mashtaka umejikita kwenye ushahidi wa kimazingira kwa sababu Lulu ndiye mtu wa mwisho kuwa na Kanumba.
Alisema ushahidi wa kimazingira unakuwa sio wa moja kwa moja, licha ya kuwa una vipande mithili ya nyololo ambavyo vimeshikana.
"Hivyo waungwana mkumbuke katika utoaji wa maoni yenu sio lazima mthibitishe makosa, pia kama mkiona mshtakiwa hausiki basi msisite kuieleza mahakama,".
Akitoa maoni yake, Mzee wa Baraza Omary Panzi amesema Lulu ameua bila kukusudia.
Amesema kuwa hatua hiyo inatokana na ushahidi wa mdogo wake Kanumba, Seth Bosco ambaye alielezea ugomvi uliotokea baina ya Lulu na marehemu.
"Maoni yangu ni kwamba marehemu alikufa kwa sababu ya kuteleza ikizingatiwa ilikuwa ni usiku na kulikuwa na giza, na chanzo cha kutekeleza ni ugomvi wake na Lulu,".
Pia Mzee wa pili, Bi.Sarah amesema Kanumba alikufa kutokana na ugomvi ambapo ushahidi pia umetueleza kulikuwa na giza.
" Hivyo Lulu hakuuwa makusudi bali aliuwa bila kukusudia, ".
Naye Mzee wa Tatu, Rajabu Mlawa ametoa maoni yake alisema kutokana na sababu zilizosomwa anaridhika na hakuna ubishi kuwa Lulu ana kosa la kuuwa bila kukusudia.
" Ameuwa bila kukusudia na nimeridhika na kilichosemwa, kwani Kanumba alikuwa na mwili mkubwa na alikuwa katika hali ya kulewa, hivyo inaonekana katika heka heka za ugomvi inawezekana Lulu alitumia nguvu kidogo ya kumsukuma Kanumba hadi kudondoka,".
Baada ya kutoa maoni hayo, Jaji Rumanyika alisema kuwa anatarajia kutoa hukumu ya kesi hiyo leo Novemba 13/2017.
No comments:
Post a Comment