Sweden yaituliza Italia, Boffuon ang'oka ....soma habari kamili na Matukio360...#share
TIMU
ya soka ya Sweden imefuzu fainali za kombe la dunia za mwaka 2018 nchini Urusi
baada ya kutoka suluhu ya bila kufungana na Italia.
Wachezaji wa Sweden wakishangilia kufuzu kombe la Dunia mwaka 2018 mara baada ya kutoka suluhu na Italia.
Matokeo
haya yanaifanya Sweden kushiriki mashindano haya tangu mwaka 2006 waliposhiriki
kwa mara ya mwisho.
Italia
ambao ni mabingwa mara nne wa kombe la dunia imeshindwa kufuzu ikiwa ni mara ya
kwanza tangu mwaka 1958.
Hii ina maana kwamba Itali
‘Azzurri’ watayakosa mashindano hayo kwa mara ya pili tokea kuanzishwa, mara ya
kwanza ilikua mwaka 1930.
Kiungo
Jakob Johansson wa Sweden aliyefunga goli katika mzunguko wa kwanza alikuwa
katika kiwango bora na kuwadhibiti vyema Italia katika uwanja wa San Siro.
Wengi
walitaraji Italia kushinda mchezo huu kwa sababu lukuki ikiwemo historia
sambamba na kucheza nyumbani.
Italia
walitawala mchezo kwa asilimia 75 na kupiga mashuti 27 lakini bahati haikuwa
upande wao.
Nusura
mshambuliaji Stephan El Shaarawy aandike bao lakini juhudi za mlinda mlango wa
Sweden Robin Olsen zilizima ndoto yake.
Kufuatia kuondolewa huko kipa mahiri wa taifa hilo, Gigga Boffuon amejiudhuru kuchezea timu hiyo.
Baadhi ya wachezaji wa Italia mara baada ya mechi na Sweden kumaliza kwa suluhu usiku wa kumakia leo
No comments:
Post a Comment