Zaidi ya watu 400 wafariki...soma habari kamili na Matukio360...#share

Na mwandishi wetu
ZAIDI ya watu 400 wamefariki na wengine zaidi ya 7,000 wamejeruhiwa katika tetemeko kubwa kukumba eneo la mpaka wa Iran na Iraq. Jitihada kubwa za uokoaji zinaendelea.

Askari wakiokoa baadhi ya watu waliofunikwa  na majengo

Makundi ya uokoaji yanatafuta manusura waliokwamwa ndani ya vifusi vya majengo yaliyoporomoka.

Tetemeko hilo la ardhi la incha 7.8 ndilo baya zaidi kutokea duniani mwaka huu.

Watu wengine waliouawa walikuwa kwenye mji ulio magharibu mwa Iran wa Sarpol-e-Zahab ulio umbali wa kilomita 15 kutoka mpaka na sehemu zingine za mkoa wa Kermanshah.

Hospitali kuu wa mkoa huo iliharibiwa vibaya na kusababisha ikubwe na matatizo ya kuwahudumia wagonjwa.

Mwanamke mmoja na mtoto waliondolewa kutoka kwa vifusi wakiwa hai kwenye mji huo, kwa mujibu wa vyombo vya habari nchini Iran.Majengo mengi katika mji huo yanaonekana kuporomoka

Huduma za maji na umeme zimekatwa katika miji mingine na baada ya majengo kuporomoka watu walilazimika kulala nje kwenye baridi.

Shirika moja la utoaji misaada lilisema kuwa watu 70,000 wanahitaji makao baada ya tetemeko hilo, na kuna ripoti kuwa maelfu ya watu huenda wakalala nje kwa usuku wa pili.

Maafisa nchini Iran wanasema kuwa watu 413 wameuawa nchi humo. Baadhi ya wanajeshi na walinzi wa mpaka ni kati ya wale waliouawa.

Nchini Iraq watu 9 waliuawa kwa mujibu wa msemaji wa shirika la msalaba mwekundu. Ofisi ya Umoja wa Mataifa nchini humo ilisema kuwa watu 500 walijeruhiwa huko na tetemeko hilo lilisikika huko Irbil, Sulaimaniya, Kirkuk, Basra na mji mku Baghdad.

Maporomoko yamefanya vigumu kwa waokoaji kufika maeneo ya vijijini na kuna hofu kuwa huenda bwawa lilo huko likapasuka baada ya kuharibiwa na tetemeko hilo. Watu wanaoishi karibu wametakiwa kuhama




About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search