Tanzania yapokea bilioni 435.7...Soma habari kamili na Matukio360...#share
Salha Mohamed
WIZARA ya Fedha na Mipango imepokea msaada wa bila riba wa
bilioni 435.79 kutoka serikali ya Sweden
Leo jijini Dar es Salaam Katibu Mkuu Wizara hiyo, Doto
James amesema wamesaini msaada wa kibajeti bilioni 53.20, msaada wa kusaidia mpango
wa elimu bilioni 235.40
Pia taasisi ya Global pertinaship imetoa milioni 94.8
kama msaada wa marekebisho ya kusaidia mpango wa kujua kusoma, kuandika na
kuhesabu.
"Wametupa msaada na wala simkopo haliwezi kuwa sehemu
ya deni la taifa, wametusaidia kwa ajili ya utekelezaji wa bajeti yetu,"amesema
Katibu Mkuu huyo
Amesema kwa mwaka wafedha 2017/2018 serikaliya Sweden itatoa msaada wa kibajeti
wa bilioni 53.20
Amesema misaada hiyo wameichambua na kwamba imetimiza matakwa
ya sheria ya misaada ya mikopo na dhamana suraya 134.
Amesema sekta ya elimu inapaswa kusimamiwa kikamilifu kwani
tangu elimu bure ianze kume kuwa na ongezeko la wananfunzi kujiunga na shule hivyo
kupitia msaada huo wameboresha mazingira ya kusomea.
Amesema katika miaka miwili, sekta ya elimu imekuwa na
maendeleo na kuwa shule 361 katika halmashauri 129 zimejengwa na zingine kukarabatiwa
na vyuo 17 vimekarabatiwa na kufungwa kopyuta 260, magodoro 6730 na viti vya kukalia
1976.
"Sekta ya elimu inachukua asilimia 18 ya fedha za
bajeti na ni sekta inayoongoza kwa kutengewa bajeti kubwa na serikali,"amesema.
No comments:
Post a Comment