EAC yatakiwa kuunga mkono sekta binafsi…Soma habari kamili na Matukio360...#share
Na Abraham Ntambara
SERIKALI za Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) zimetakiwa
kushirikiana na sekta binafsi ili kufanikisha mapinduzi ya viwanda.
Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan akiwa katika picha ya pamoja baada ya ufunguzi wa Baraza la wafanybiashara na Wajasiliamali wa Jumuiya ya Afrika Mashariki jijini Dar es Salaam.
Ombi hilo limetolewa leo jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi
Mtendaji wa IBM holdings, Tanzania Felix Mosha katika ufunguzi wa mkutano wa
siku tatu wa Baraza la Wafanyabiashara na Wajasiliamali wa EAC.
“Ushirikiano wa sekta binafsi na serikali za EAC utafanikisha
kuleta mapinduzi ya viwanda,” amesema Mosha.
Aidha amezitaka kuwekeza katika miundombinu kama ya barabara,
reli na umeme na teknolojia ili kuwasaidia wafanyabiashara katika
kuwarahisishia shughuli zao.
Ameongeza kwa kuomba kuondolewa kwa vikwazo mipakani, laikini
pia kuhakikishiwa usalama kwani hakuna mfanyabiashara wala mwenyekezaji anayeweza
kuwekeza mahali pasipo na usalama.
Kwa upande wake Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan ambaye
alikuwa mgeni rasmi, amesema serikali itahakikisha inashirikiana na
wafanyabiashara kwa kuwahakikishia usalama lakini pia kusimamia sheria.
Pia amesema itaboresha miundombinu ya barabara, reli na umeme
ili kusaidia katika kuongeza uzarishari pamoja na upatikanaji wa soko.
Aidha amewataka wadau katika mkutano huo kujadili changamoto
mbalimbali zinazokabili sekta hiyo katika EAC ili waje na mapendekezo ambayo
yataboresha katika kusaidia sekta ya viwanda.
Aliwahakikishia kuwa serikali itaendelea kushirikiana kwa
nguvu zote katika yale yote yaliyokatika bakubaliano ndani ya Jumuiya.
Lengo la mkutano huo ni kujadili changamoto zinazowakabili wafanyabiashara wa EAC na jinsi ya kuzitatua ili kusaidia katika mapinduzi ya viwanda.
No comments:
Post a Comment