Uamuzi kesi ya Mobeto dhidi Diamond kesho...soma habari na Matukio360..#share
Na mwandishi wetu
MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi
Kisutu upande wa Watoto kesho inatarajiwa kutoa uamuzi kama kesi iliyofunguliwa
na mwanamitindo, Hamisa Mobeto dhidi ya mwanamuzi, Nassib Abdul 'Diamond Platnum' itupiliwe
mbali ama la.
 Msanii wa muziki, Nassib Abdul 'Diamond Platnum
Uamuzi
huo  unatarajiwa kutolewa na Hakimu
Devotha Kisoka wa mahakama hiyo. Hakimu
Devotha atatoa uamuzi huo baada ya kusikiliza hoja za pande hizo mbili
husika  kutokana na msanii Diamond
kuwasilisha pingamizi dhidi ya kesi hiyo iliyofunguliwa na Mobeto.
Kwa
mujibu wa pingamizi lililowasilishwa na 
Diamond  mahakamani hapo anadai
kuwa  kesi hiyo imefunguliwa kwa kutumia
kifungu ambacho si sahihi.  Hoja ambayo
ilipingwa na Mobeto.
Mobeto
alifungua kesi hiyo mahakamani hapo, pamoja na mambo mengine anaomba matunzo ya
mtoto waliozaa na msanii Diamond.
Mobeto  anaiomba mahakama imwamuru Diamond kutoa matunzo
ya mtoto ya kila mwezi. Alifungua kesi hiyo kupitia mawakili wake Abdullah
Lyana na Walter Godluck kutoka kampuni ya uwakili ya Century Attorneys.
Kupitia
hati hiyo ya madai, Mobeto  anaomba
Diamond amuombe msamaha kwa kumsababishia madhara yaliyoishtua familia yake.
Diamond aliwasilisha hati ya majibu hayo
kinzani akipinga maombi hayo ya Mobeto 
akidai  gharama anazodai kulipwa
kwa mwezi ya milioni 5 kwa ajili ya matunzo ya mtoto ni kubwa  na hawezi kuzimudu. 




No comments:
Post a Comment