'UPDATES' Mtoto wa Chacha Wangwe alipa faini aachiwa huru ...soma habari kamili na Matukio360...#share
Na
Abdulrahim Sadiki
BOB
Chacha Wangwe ambaye ni mtoto wa
mwanasiasa marehemu Chacha Wangwe, amenusuruka kifungo cha mwaka mmoja na nusu jela
baada ya kulipa faini ya milioni 5.
Mapema
leo Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu ilimuhukumu BOB Chacha Wangwe kulipa faini
ya milioni 5 ama kutumikia kifungo cha
mwaka mmoja na nusu jela.
Ni
baada ya kupatikana na hatia katika shtaka la kuchapisha taarifa za
uongo kwenye mitandao ya kijamii.
Hakimu
Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi alitoa hukumu hiyo leo baada ya kupitia ushahidi
uliotolewa na mashahidi sita wa upande
wa mashtaka, vielelezo 5 na utetezi wa mshtakiwa mwenyewe.
Amesema
kuwa Mei 7, 2016 askari polisi walipata taarifa ya chapisho la mtoto huyo wa
Chacha Wangwe, Bob ambapo walianza kumfuatilia na kumkamata kisha walichukua
simu na kuipeleka maabara ya Polisi ili kuikagua.
Bob
hukupinga kuandika maneno hayo lakini umedai kuwa hakuyachapisha katika mtandao
wa kijamii bali yalikuwa ni siri kwenye akaunti yake.
Hakimu
Shaidi alisema kuwa wakati wa ushahidi imeelezwa kuwa simu yake ilipokaguliwa
ilionekana ilitumika kuchapisha ujumbe huo kwa jamii na watu walijibu,
ikiashiria ujumbe uliwafikia.
Nidhahiri
ulikuwa na nia ya kuchapisha taarifa hiyo, kueleza kile ambacho ulikiona sahihi
kama ingekuwa ni ujumbe wako binafsi basi polisi wasingeweza kukutafuta, na
watu wasingekujibu.
Hakimu
Shahidi alisema kutokana na hatua hiyo Bob alokutwa na hatia chini ya kifungu cha 16 cha sheria
ya makosa ya mtandao ya mwaka 2015.
Bob
aliomba apunguziwe adhabu kwa sababu ni mwanafunzi wa masomo ya sheria, pia ni
kijana mdogo na ni kosa lake la kwanza
kulitenda.
Hakimu
Shaidi alisema anakubaliana na hoja za Bob, kwani mahakama inamuona bado ni
mdogo na anapaswa kufanya mambo mengi mazuri katika jamii.
Pia
amesema kama yeye ni mwanafunzi wa masomo ya sheria anapaswa kufanya mambo mema
katika jamii vitu ambavyo wengine watamuiga.
No comments:
Post a Comment