Mugabe ang'olewa urais Zimbabwe ...soma habari kamili na Matukio360...#share
Na mwandishi wetu
EMERSON Mnangagwa ametangazwa kuwa rais wa mpito nchini Zimbabwe kwa tiketi ya chama cha ZANU-PF.
EMERSON Mnangagwa ametangazwa kuwa rais wa mpito nchini Zimbabwe kwa tiketi ya chama cha ZANU-PF.
Emerson Mnangagwa
Mnangagwa alikuwa makamu wa rais wa zamani wa nchi hiyo chini ya Rais Robert Mugabe.
Kwa mujibu wa taarifa ya chama cha ZANU-PF, inasemama Mnangagwa amefanywa kuwa rais wa
mpito.
Hivi karibuni Mnangawa mwenye umri wa miaka 75 alifutwa kama makamu wa rais kutokana
na kile serikali ilisema kuwa kutokuwa mtiifu.
Kufutwa kwake kulionekana kama nia ya kumwezesha mke wa rais Mugabe,
Grace kufuata nyayo za mumewe na kuwa kiongozi wa Zimbabwe.
Awali alikuwa ametoa wito kwa mumewe kumfuta makamu wa rais.
Mnangagwa ambaye ni mkuu wa zamani wa ujasusi amekuwa mtu ambaye
alitarajiwa kumrithi rais Mugabe 93.
Kufutwa kwake kulimaanisha kuwa Grace Mugabe anatarajiwa kuteuliwa kuwa
makamu wa rais wakati wa mkutano maalum wa chama tawala cha Zanu-PF mwezi ujao.
No comments:
Post a Comment