Video: Rais Magufuli kufanya ziara ya siku nne mkoani Kagera.. soma taarifa kamili na matukio360.. #share

Rais  John Pombe  Magufuli  atawasili  Mkoani  Kagera  siku  ya  Jumatatu 6/11/2017 kwa  ziara  ya  kikazi  mpaka  9/11/2017.

Rais Magufuli katika picha mojawapo kutoka maktaba

Tarehe  6/11/2017 Katika  Manispaa  ya  Bukoba  saa nane  mchana  atazindua  rasmi  uwanja  wa  ndege  wa  Bukoba  na  baada  ya  hapo  atakuwa  na  mkutano  wa  hadhara  na  kuongea  na  wananchi katika  eneo  la  uwanja  wa  ndege  Bukoba,

(Video chini: Rais Magufuli akiwa amebarizi anasikiliza wimbo wa kabila la Wasukuma pamoja na Mama yake mzazi Suzana Magufuli (kushoto) na Dada yake Mkubwa Monica Joseph Magufuli (kulia))

 7/11/2017 asubuhi  ataelekea  wilaya  ya  Karagwe  na  atazindua  barabara  eneo  la kihanga (kishoju ) 8/11/2017 asubuhi  atatembelea  kiwanda  cha  sukari  Kagera  sugar  wilaya  ya  Missenye  atatembelea  mashamba  ya  miwa  na  kutembea  kiwanda, na  atakutana  na  wafanyakazi  na  uongozi, 9/11/2017 Rais  Magufuli  na  Rais  Museveni  wa  Uganda  watazindua  majengo  ya  Forodha  katika  mpaka  wa  Mutukula  na  wote  wawili  watazungumza  na  wananchi.

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search