Katibu Chadema, wenzake 11 mbaroni kwa kumshambulia mgombea CCM...Soma habari kamili na Matukio360...#share

Na Mwandishi Wetu
KATIBU wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) wilaya ya Arusha,
Innocent Kisanyanga na wafuasi wengine 11 wa chama hicho wanashikiliwa na Jeshi
la Polisi Mkoani humo kwa kosa la kumshambulia mgombea udiwani wa Chama
cha Mapinduzi (CCM) Kata ya Muriet, Francis Mbise.
RPC Charles Mkumbo
Mbali na kushikiliwa Kwa wafuasi hao pia jeshi hilo linashikilia
gari la matangazo la chama hicho ambalo limekuwa likitumika kutangaza mikutano
ya Chadema katika kampeni za uchaguzi mdogo jijini hapa.
Kamanda wa jeshi la polisi mkoani Arusha, RPC Charles Mkumbo
amethibitisha kushikiliwa kwa wafuasi hao na kusema kwamba walikamatwa jana
usiku katika eneo la FFU kwa Morombo
Amesema kwamba wafuasi hao waliwavamia wafuasi wa ccm wakati wakitoka katika mikutano ya kampeni eneo la Muriet na kuanza kuwashambulia .
Ameeleza kuwa katika vurugu hizo wafuasi hao walimshambulia Mbise na
kumuumiza sehemu mbalimbali za mwili wake hali iliyofanya akimbizwe hospitalini kwa ajili matibabu.
Amewataja wanaoshikiliwa kuwa ni Edwin Christopher, Yohana Mtaa, Paschael Lucas, Nasoro Ally, Godson Samwel, Joram Baraka, Bayo Shana, Cecilia Lucas, Aurelia Lucas ,Rehema Juma, Amina Musa sanjari na InnocentKisanyage.
Kamanda Mkumbo amesema kwamba jeshi lake bado linaendelea na uchunguzi wa tukio hilo na pindi uchunguzi utakapokamilika watafikishwa mbele ya vyombo vya sheria kujibu mashtaka yanayowakabili

No comments:
Post a Comment