Viongozi ACT wahojiwa kwa saa sita...Soma habari kamili na Matukio360..#share
Na Abraham Ntambara
VIONGOZI wa Chama cha ACT-Wazalendo wamehojiwa na Jeshi la Polisi katika Kituo cha Makosa ya
kifedha, Kamata jijini Dar es Salaa kwa
takribani saa sita.
Mwenyekiti wa Chama cha ACT-Wazalendo Yeremia Maganja akizungumza na waandishi wa habari baada ya mahojiano na Jeshi la Polisi katika Kituo cha Makosa ya kifedha, kamata jijini Dar es Salaa.
Waliohojiwa ni Katibu Mkuu wa Chama hicho Doroth Semu na Mwenyekiti Yeremia Maganja kwa
niaba ya Kamati Kuu ya chama ambao walianza kuhojiwa saa 3:30 asubuhi hadi saa
9:15 alasiri.
Akizungumza na waandishi wa habari baada ya mahojiano hayo, Maganja
amesema wamehojiwa kuhusiana na kamati kuu kuchambua na kuiandaa taarifa ya kina ya Takwimu za Serikali juu ya hali ya
uchumi wa nchi kusinyaa kinyume na Kifungu cha 37(5) ya Sheria ya Takwimu 2015.
"Kwa kuwa tumeambiwa tunatuhumiwa, basi tumekubaliana na tumetoa maelezo yetu, na tumemueleza mwakilishi wa DCI kwamba wajumbe wa Kamati Kuu wanatoka nchi nzima na ni wahali ya kawaida wa maisha ya kawaida hatuwezi kukusanyika kwa siku mbili tatu wakaweza kufika kwa hiyo wametuelewa kwamba ni vigumu kuwakusanya kwa wakati mmoja ndani ya siku nne wakawa wamefika," amesema Maganja.
Aidha amesema kutokana na ugumu wa kuwakusanya wajumbe wote wa kamati na kuripoti polisi kama witoulivyokuwa ukiwataka wameacha namba za
simu na majina ya wajumbe wa kamati kwa Mkurugenzi Msaidizi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI) ili kama watawahitaji wawatafute.
Maganja ameongeza kuwa wametakiwa kuripoti tena kituoni hapo
Novemba 26, 2017 kwa ajili ya kujua hatua nyingine zaidi zitakazofuata.
Awali Kiongozi wa Chma hicho Zitto Kabwe akizungumza na
waandishi wa habari baada ya kufika katika kituo hicho cha Makosa ya Kifedha
cha Kamata akitokea kituo cha Polisi Chang'ombe majira ya saa 5 asubuhi
alipokuwa ameripoti kwa ajili ya kujua
hatma yake ikiwa atafikishwa mahakamani au vinginevyo, amesema kuwa ametakiwa kurudi
kituoni hapo November 17,2017.
Kiongozi wa Chama cha ACT-Wazalendo Zitto Kabwe akizungumza na waandishi wa habari baada ya kutoka kituo cha polisi cha Chang'ombe jijini Dar es Salaam.
Pia amesema anatakiwa kuripoti kesho polisi katika Kituo cha Makosa ya kifedha, kamata jijini Dar es Salaa kwa ajili ya mahojiano na DCI
"Chang'ombe wanasubiri hati ya mashtaka kutoka kwa DPP
na kama upelelezi upo tayari wataangalia uwezekano wa kunipeleka
mahakamani, lakini pia kesho nimetakiwa kuripoti hapa," amesema Zitto.
Zitto ameongeza kuwa ikiwa suala hilo litapelekwa mahakamani
itakiwa ni kesi ya kwanza ya namna hiyo katika historia nchini kuhusu masuala ya Takwimu ya Taifa kupelekwa
mahakamani.
Ameongeza kuwa wao wamejipanga kwa kuwa na wanasheria pamoja na
wataalamu wa masuala ya uchumi ili kukabiliana na kesi hiyo na wanaamini mahakama
ndiyo itatoa tafsiri ikiwa kwa kutoa takwimu hizo wamekosea kwani walichofanya
wao ni uchambuzi wa takwimu zilizotolewa na Mamlaka husika.
Aidha amesema wanafikiria kufungua kesi ya kutaka kuondoa vipengele
vyote vya Sheria ya Takwimu nchini, vinavyozuia uhuru wa watu wengine kufanya
uchambuzi na kutoa maoni yao juu taarifa hizo.
No comments:
Post a Comment