Wajue mawakili ‘feki’...soma habari kamili na Matukio360...#share
Na Salha Mohamed
WANANCHI wanaohitaji uwakilishi mahakamani wametakiwa
kujiridhisha uhalali wa wakili kama amesajiliwa kwa Msajili wa Mahakama Kuu ili
kuepuka kutapeliwa na mawakili ‘feki’.
Wakili wa kujitegemea, Leonard Manyama
Mojawapo ya madhara, ikigundulika wakili hana sifa hata kama umeshinda kesi, hukumu hiyo ufutwa hali ya kuwa ameshamlipa fedha nyingi
Hayo
yamesemwa Dar es Salaam na mwanasheria
ambaye pia ni wakili wa kujitegemea, Leonard Manyama wakati akitoa ufafanuzi wa
kisheria wa mtu wa kumuona ili kuwawakilisha mahakamani au kwenye vyombo vya
haki kama mawakili wa kujitegemea.
Amesema
si kila mwanasheria ni wakili na anamamlaka
ya kuwasimamia watu mahakamani na kwenye mabaraza mbalimbali.
"Mwenye
sifa ya kumuwakilisha mtu mahakamani kama wakili wa kujitegemea anapaswa kuwa na
sifa tatu, "amesema.
Amesema
sifa hizo ni kwa mujibu wa kifungu cha 39 cha sheria ya mawakili sura namba
341.
Amesema
moja ya sifa hizo ni jina lake kuwepo kwenye kitabu maalum cha mawakili ambacho
kinatunzwa na msajili wa mahakama kuu.
"
Kitabu hicho kinahifadhiwa na msajili wa mahakama Kuu na ndiyo anayo majina
yote a mawakili nchini ambao wanauhalali wa kuwawakilisha watu mahakamani,
"amesema.
Ameongeza
kuwa ili mtu aingie kwenye orodha hiyo anapomaliza masoma ya sheria (law school)
anatakiwa kuapishwa na Jaji Mkuu na kupewa cheti cha uwakili.
Amesema
sheria inasema mtu huyo anapaswa kuwa na
cheti halali cha uwakili kinachomruhusu kuhudhuria mahakamani.
Amesema
sifa nyingine ni kuwa na leseni halali
ya kibiashara iliyoambatanishwa
na nyaraka za maombi ya kupata leseni ya kufanya kazi kama wakili.
"
Yeyote ambaye hana vigezo hivi haruhusiwi kwa mujibu wa sheria kumuwakilisha
mtu yeyote mahakamani, "amesema.
Amesema
kufanya hivyo ni kosa kisheria kwa mujibu wa kifungu cha 41 na 42 cha sheria ya
mawakili sura ya 341.
Kinachoeleza
kuwa ni kosa kisheria kwa mtu yeyote
ambaye hatambuliki na msajili wa mahakama Kuu kwenda mahakamani kumuwakilisha
mtu au kuandaa nayaraka za kisheria.
Amesema
endapo wakili akigundulika hana sifa na hata kama umeshinda kesi, hukumu hiyo ufutwa hali ya kuwa amelipa fedha nyingi za kuendesha kesi.
Amesema
kosa hilo ni la jinai na adhabu yake kifungo cha miezi sita.
"Lakini
sheria pia inasema mtu huyo anaweza akapelekwa mahakamani na adhabu yake ni faini
isiyopungua na iliyozidi milioni moja au
kufungwa jela miezi 12 au vyote kwa pamoja, "amesema.
No comments:
Post a Comment