Hatma ya Mugabe leo, wananchi wapiga kambi Ikulu...soma habari kamili na Matukio360...#share
Na
mashirika ya kimataifa
WAKATI
waandamaji nchini Zimbabwe wakiweka kambi nje ya ofisi ya rais Mugabe
wakishinikiza ajiuzulu, leo vikao viwili kwa nyakati tofauti vinakutana kujadili
hatma ya kiongozi huyo.
Waandamanaji nchini Zimbabwe wakiweka kambi nje ya ofisi ya rais Mugabe kumshinikiza kujiuzulu
Mapema
hii leo Mugambe atakutana tena na mkuu wa majeshi, Jen Constantino Chiwenga na baadaye
watendaji wakuu wa chama chake cha ZANU-PF
Wapiganiaji
wa uhuru ambao hadi kufiki mwaka jana walikuwa watiifu kwa rais Mugabe pia
wanasema kwamba rais Mugabe anafaa kung'atuka mamlakani.
Kiongozi wa shirika hilo amewataka raia kuelekea
katika makao ya rais Mugabe.
Juzi
mara baada ya kikao chake na mkuu huyo wa majeshi, Mugabe alionekana hadharani kwenye
mahafali ya moja ya chuo kikuu mjini
Harare Zimbabwe.
Jana
waandamanaji nchini humo walielekea
katika afisi ya rais Mugabe ili kumtaka kujiuzulu.
Maandamano
hayo yanajiri kufuatia furaha ilioonekana miongoni mwa raia baada ya jeshi
kuingilia kati na kumzuia rais Mugabe kwa muda nyumbani kwake siku ya Jumatano.
Wanajeshi
katika ikulu ya Whitehouse walioonekana wakiwarudisha nyuma waandamanaji.
Jeshi
liliingilia kati baada ya rais Mugabe kumfuta kazi makamu wake wa urais,
akionyesha ishara za kutaka mkewe kumrithi.
Mugabe mwenye umri wa miaka 93 ameiongoza
Zimbabwe tangu ilipojipatia uhuru kutoka kwa Uingereza 1980.
Jeshi
limehakikisha kuwa anaendelea kukaa katika makoa yake huku likidai kujadiliana
naye na kwamba litatangaza kwa wananchi matokeo ya mazungumzo hayo hivi
karibuni.
Nje
ya ikulu ya rais kuna baadhi ya watu walioketi chini ili kuonyesha pingamizi
yao mbele ya majeshi, huku kiongozi wa upinzani, Morgan Tsvangirai akihutubia
umati mkubwa.
No comments:
Post a Comment