Mkuu wa Wilaya: Wanawake acheni kutumia vipodozi vyenye sumu...Soma habari kamili na Matukio360...#share

Na Salha Mohamed

MKUU wa Wilaya ya Ilala, Sophia Mjema amewaasa wanawake kuacha kutumia vipodozi vyenye viambato sumu na  watumie vipodozi vya asili ili kujiepusha na saratani.
Mkuu wa wilaya ya Ilala Sophia Mjema akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam.

Mjema ameyasema hayo jijini Dar es Salaam, wakati wa ufunguzi wa kampeni ya Afya na Urembo iliyoandaliwa na Kampuni ya Timeless.

Amesema wapo wanawake wanaotumia vipodozi vyenye viambato sumu ambapo amewataka kupitia mafunzo watakayopata kuwa mabalozi kwa wengine.

"Sasa hivi saratani ni nyingi kwasababu hutujui aidha ni sababu y tunavyokunywa au kupaka, "amesema.

Amesema kupitia kampeni hiyo aliyozindua wanapaswa kuwa mabalozi kwa kutoa elimu ili vipodozi vyenye viambato sumu visiendelee kwani bado watu wanauza.

" Mnajua serikali yetu inakemea vipodozi vyenye viambato sumu, vinavyowaumiza wakinamaa na wakina baba kupitia elimu mtakayotoa itasaidia itasaidia wanawake kutokuwa na rangi mbili, "amesema.

Amesema serikali ipo tayari kuwasaidia kutengeneza bidhaa za asili kwani serikali inapiga marufuku matumizi ya vipodozi ambayo si rafiki kwa mwili wa binadamu.

Kwa upande wake mkurugenzi wa Timeless, Irene Moshi amesema  kampeni hiyo itakuwa endelevu nchi nzima a itatoa ajira kwa vijana.

"kampeni hii itaelimisha na kujifunza kwa pamoja ni namna gani vipodozi vitumike kwao kuwaona kwa watoa huduma, "amesema.

Amesema wapo wanawake waliokuwa na saluni huku akiwa hana utaalamu kupitia kampeni hiyo wamepata na wataweza kutoa huduma nzuri.

Mkuu wa Idara ya huduma za Kinga na Kinywa kutoka Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Dk. Rachel Mhavile wakati akitoa mada ya usafi wa kinywa amesema  wanawake hasa wajasiliamali wanapaswa kuwa na kinywa safi.

"Afya y kinywa na meno inamawasiliano na afya ya mwili,  harufu mbaya ya kinywa ni fedheha na aibu...madaktari tupo wengi mkapate ushauri, "amesema.

Amesema takwimu zinaonesha watu wengi hupiga mswaki mara moja kwa siku ambapo mtu anatakiwa kupiga mswaki mara mbili kwa siku na dawa yenye madini ya Floride kwa ulinzi w meno. 

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search