ACT kutoshiri uchaguzi ubunge na udiwani wa Januari...soma habari kamili na matukio360..#share
Na Abraham Ntambara, Dar es salaam
CHAMA cha ACT Wazalendo kimetangaza kutoshiriki
uchaguzi wa marudio wa ubunge katika majimbo matatu na udiwani katika kata sita wa Januari 13, 2018.
Kimetoa msimamo huo leo na kwamba hatua yake hiyo ni
kutokuwapo kwa mazingira sawa na huru ya kidemokrasia na uchaguzi. Majimbo hayo ni Singida Kaskazini, Songea Mjini na Longido Kaskazini
Kaimu mwenyekiti wa ACT Wazalendo Yeremia Mangaja katikati, kushoto kwake ni kiongozi mkuu wa chama hicho, Zitto Kabwe
Akitangaza uamuzi huo leo jijini Dar es salaam kamimu mwenyekiti
taifa wa ACT, Yeremia Maganja amesema uamuzi wao umezingitia mambo
matano
ambayo kimsingi yaliyojitokeza kwenye uchaguzi wa udiwani Novemba 2017.
Sababu hizo ni:
I. CCM na Serikali yake kiliongeza matumizi ya mabavu
kupitia vyombo vya dola hasa jeshi la polisi ili kuweka mazingira ya kushinda
uchaguzi
II. Chama Tawala kilihakikisha kinawatumia vyema
watendaji wa halmashari wanaohusika na usimamizi wa uchaguzi ambao wengi
waliteuliwa kwa misingi ya ukada kwa Chama hicho ili kujihakikishia ushindi.
III. Mazingira yalipoonekana dhahiri kuwaelemea, Chama
Tawala walitumia njia za kimabavu Kama vile kuvamia viongozi, kuteka viongozi,
au kuwaweka mahabusu viongozi na mawakala
IV. Kila mbinu ilipoonekana kugonga mwamba, kwenye
maeneo kadhaa, Chama Tawala, kwa kutumia vyombo vya dola kiliamua kujitangazia
ushindi kimabavu licha ya matokeo kuonesha kuwa wameshindwa
V. Tume ya Taifa ya Uchaguzi, NEC ilionekana kutojali
kabisa hitilafu zilizojitokeza na kuchukua hatua kurekebisha kabla ya kuitisha
Uchaguzi Mpya.
“Ni dhahiri kwamba uwanja wa demokrasia nchini
umevurugwa sana na mchakato mzima wa uchaguzi huru na wa haki kuharibiwa
kabisa. Hivyo basi, Kamati Kuu ya Chama chetu imeazimia kuwa Chama chetu
KISISHIRIKI kwenye uchaguzi ujao wa marudio wa tarehe 13 Januari 2018,’’
amesema Maganja.
Hata hivyo mwenyekiti huyo amesema wanatambua kutoshiriki chaguzi tu haitoshi kwani haijibu
swali la nini kinafuata baada ya kususia hivyo watafikia wadau wote wa
Demokrasia nchini na kuweka mikakati ya pamoja ya hatua za ziada za kuchukua
ili kuboresha mazingira ya chaguzi za haki nchini pamoja na kuweka shinikizo
kubwa kwa Serikali kufanya mabadiliko muhimu ya kisheria, kiutendaji na
kikatiba ili kuweka sawa uwanja wa mapambano ya Kidemokrasia.
“ ACT itavitembela
na kuanzisha mazungumzo na Vyama vyote vya upinzani ili kuona njia bora zaidi
ya kimapambano ya pamoja katika kukabiliana na vitendo vya sasa vya Chama
Tawala cha kuvuruga uchaguzi huru na wa haki,"
"Chama pia kitautumia muda wa
sasa na mwezi Januari Kama kipindi cha kushirikiana na Vyama vya wafanyakazi na
wafanyakazi wenyewe kupambana dhidi ya Muswada wa Sheria ya Pensheni ambao
utawakosesha pensheni malaki ya wafanyakazi wa sekta ya umma hasa walimu kama
utapitishwa kama ulivyo.
"Hatua hizi pia zitahusisha
makundi ya walio kwenye sekta isiyo rasmi, kama wakulima, wavuvi, wamachinga,
wajasiriamali nk, ambao sheria hii inawaacha nje kabisa.’’
No comments:
Post a Comment