Babu seya, Papi kocha waachiwa huru, 61 kutonyongwa...soma habari kamili na matukio360...#share

Na mwandishi wetu
RAIS John Magufuli ametoa msamaha wa kuachiwa
huru kutoka jela kwa familia ya Nguza
Vikingi na wafungwa 61 kutonyongwa.
Pia ametoa msamaha kwa wafungwa 8157, kati ya hao 1828
ameagiza kuachiwa huru leo na waliobaki
wamepunguziwe muda wa vifungo vyao.
Rais John Magufuli
Ametoa agizo hilo leo mjini Dodoma katika maadhimisho
ya miaka 56 ya uhuru wa Tanzania Bara.
“Nimetoa msamaha wa kuachiwa huru leo hii kwa familia
ya nguza Vikingi(Babu Seya) na John Nguza(Papii Kocha). Pia nimetoa msamaha wa
kutonyongwa na kuachiwa huru watu 81 waliokuwa miongoni mwa wafungwa
waliotakiwa kunyongwa,’’ amesema Magufuli na kuongeza
“Nimewasamehe wafungwa 8157, kati ya hao 1828 waachiwe
huru leo, waliobaki nimewapunguzia muda wa vifungo vyao.”
Amesema hatua yake hiyo imezingatia mamlaka aliyopewa
na katiba kwa mujibu wa ibara ya 45.
Amesema Tanzania inajumla ya wafungwa takribani
39,000, kati yao wanaume ni 37,000 na wanawake 2000.
Amesema jumla
ya wafungwa 666 wamehukumiwa kifungo cha maisha jela huku wanawake wakiwa ni 11.
“Katika idadi ya waliohukumiwa kunyongwa wanawake ni
19,’’ amesema Magufuli
Amesema kwa mujibu wa idadi ya wafungwa wanaume ni
wengi hivyo wajitafakari kwa nini wao ni wengi.
Rais Magufuli amesema mbali na mamlaka aliyopewa kwa
mujibu wa katiba, uamuzi wake umezingatia sababu mbalimbali ikiwamo umri,
nidhamu na muda waliokaa wafungwa jela.
“Wapo wafungwa waliohukumiwa
kunyongwa wana umri zaidi ya miaka 85, wamekaa
zaidi ya miaka 45 jela na wapo waliotubu
makosa yao.
Binadamu wote tunaomba kusamehewa na hata mimi nimeomba
kusamehewa na nimeguswa na hili. Wengi wao hawakuua albino wala hawakuwa
majambazi, hivyo ninatoa msamaha huo,’’ amesema rais
“Yupo aliyefungwa akiwa na miaka 18 na sasa anamiaka
zaidi ya 60, huyu anaitwa mzee Maganga Matonya anamiaka 85 amekaa gerezani
miaka 37 baada ya kuhukumiwa na alikaa mahabusu miaka 7 ni muhimu nikampa msamaha wa kuachiwa huru,’’
Miongoni mwa magereza yaliyokuwa na wafungwa waliokuwa
wamehukumiwa konyongwa na sasa wamepata msahama wa kutonyongwa ni Uyui Tabora
wafungwa wawili, Dodoma Isanga wafungwa 15,
Tanga Maweni wafungwa 11, Morogoro Kinguruwila wafungwa 15 na Dar es Salaam Ukonga wafungwa 19.
No comments:
Post a Comment