Magufuli mgeni rasmi uzinduzi ASDP II...soma habari kamili na matukio360...#share

Na
Abraham Ntambara, Dar es Salaam
RAIS
John Magufuli anatarajia kuwa mgeni rasim katika uzinduizi wa programu ya
kuendeleza sekta ya kilimo awamu ya pili (ASDP II) Juni 4, 2018.
Waziri wa Kilimo Dk. Charles Tizeba akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) jijini Dar es Salaam.
Akizungumza
na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam Waziri wa Kilimo Dk. Charles
Tizeba amesema programu hiyo inajumuisha
wizara za kisekta ambazo ni wizara ya kilimo, mifugo na uvuvi, Ofisi ya Rais
Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi) viwanda, biashara na uwekezaji,
wizara ya ardhi, nyumba, maendeleo ya makazi na wizara ya maji na umwagiliaji.
“Lengo la programu
hii ni kuleta mageuzi katika sekta ya kilimo ili kuongeza uzalishaji na tija
katika kilimo, mifugo na uvuvi, kuongeza pato la wakulima wafugaji na
wavuvi na kuongeza pato la taifa na kuwa na uhakika wa usalama wa chakula na
lishe,” amesema Dk. Tizeba.
Aidha
Dkt Tizeba amesema kuwa ASDP II itatekelezwa katika mikoa na wilaya kwa
kuzingatia mazao ya kipaumbele kufuatana na ikolojia ya kilimo ya kanda kwa
miaka kumi 10 kwa vipindi viwili vya miaka mitano mitano ambapo kipindi cha
kwanza kitaanza 2018/19 hadi 2023/24.
Amebainisha
kwamba washiriki wa programu hiyo ni
wadau mbalimbali wa sekta ya kilimo, mifugo, uvuvi, ushirika,wizara,Taasisi za
serikali na zisizo za serikali, sekta binafsi pamoja na wananchi wote
Katika
hatua nyingine waziri Tizeba amekanusha
taarifa za kuwa alitengewa bajeti ndogo katika wizara yake katika mwaka wa
fedha wa 2018/19 katika bunge la bajeti na kudai bajeti yake iko vizuri na
spika wa bunge alikuwa anatania kwani yeye ni mtani wake.
No comments:
Post a Comment