Chadema yatoa neno mbunge wake kujiuzulu...soma habari kamili na matukio360...#share
Na Mwandishi Wetu
CHAMA cha Demokrasia na
Maendeleo (Chadema) kimeshangazwa na hatua ya aliyekuwa mbunge wa Siha kupitia
chama hicho Dk Godwin Mollel kujiuzulu nafasi hiyo na kujiunga na Chama cha
Mapinduzi (CCM) kwa kile alichodai ni kwa ajili ya kutetea rasilimali za taifa.
Mwenyekiti wa Chadema Freeman Mbowe
Kwa mujibu wa taarifa
iliyotolewa jioni hii kwa umma na Mkurugenzi wa Itikadi, Mawasiliano na Mambo
ya Nje wa Chadema John Mrema imesema “Ni jambo la kushangaza kwa kuwa kitendo
chake cha kulikimbia Bunge kama chombo cha kusemea na kutetea rasilimali za
Taifa na kuja uraiani inatoa taswira gani maana kalikimbia Bunge lenye wajibu
huo kwa mujibu wa Katiba na Sheria za nchi yetu,” amesema.
“Tunawashauri wale wote ambao wanajitoa waeleze sababu halisi na
sio kuhadaa umma kwa sababu uchwara kama hizi, maana wapo wanaosema wanaacha
kazi kwenda kuunga mkono dhana ya 'hapa kazi tu' na wengine wanasema wanaenda
kuunga mkono juhudi za kuboresha maisha kwa kuacha kazi,” ameongeza.
Amesema Chadema kimepokea taarifa ya kujiuzulu kwa mbunge huyo na kuhamia CCM kupitia
mitandao ya kijami.
Mrema ameeleza sababu hiyo aliyotoa ni ya kushangaza kwani Bunge ndicho chombo chenye
wajibu wa kusimamia na kulinda rasilimali za Taifa kwa niaba ya wananchi.
Amebainisha kuwa wako imara na wataendelea na ajenda zao bila
kuyumbishwa na wimbi hili la watu wachache ambao wameamua kuwasaliti wapiga
kura wao kwa kutoa sababu zisizo za msingi ambazo hazina maslahi kwa Taifa bali
kwa maslahi yao binafsi . Huu ni ubinafsi wa hali ya juu.
Amesema wataendelea kujenga taifa letu na chama bila kujali njaa za baadhi yao wala maslahi ya
watu wachache na kuongeza kwamba wale wenye dhamira thabiti ndio wataweza
kufika mwisho wa safari ya kuleta mabadiliko salama.
Amesema ni dhahiri wale
waliotanguliza ubinafsi hawataweza kufika nao mwisho wa safari hii.
No comments:
Post a Comment