Ulipaji kodi Zanzibar sasa kwa simu...soma habari kamili na matukio360..#share
Na Mwajuma Juma, Zanzibar
KAMPUNI ya simu za Mkononi ya Zantel imetiliana saini na Bodi ya Mapato Zanzibar (ZRB) kwa ajili ya ulipaji wa kodi kwa kutumia njia ya mtandao kupitia huduma ya Easy Pesa.
Utiaji saini huo umefanyika leo katika ofisi za ZRB Mazizini nje Kidogo ya Mji wa Zanzibar, ambapo kwa upande wa Zantel iliwakilishwa na Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni hiyo Sheref El-Barbery na ZRB ni Kamishna wa bodi hiyo Amour Hamil Bakir.
Akizungumza mara baada ya utiaji wa saini hiyo Kamishna wa Bodi ya Mapato Zanzibar (ZRB) Amour Hamil Bakir amesema huduma hiyo inafanyika ili kuwarahisihia wateja wao katika ulipaji wa kodi ambao wamekuwa wakitumia gharama nyingi kufata huduma hiyo ofisini.
Amesema huduma hiyo imewalenga zaidi wafanyabiashara wadogo.
Mkurugenzi Mkuu wa Zantel Sheref El-barbery amesema ni matarajio yao kwamba huduma hiyo itarahisisha ulipaji kodi kwa kufanya malipo ukiwa popote.
Amewataka wafanyabiashara kutumia huduma hiyo ambayo itakuwa ni rahisi kwao katika ulipaji wa kodi na kuwapunguzia gharama walizokuwa wakizitumia wakati wa kufata huduma hiyo makao makuu .
No comments:
Post a Comment