George Weah rais mteule wa Liberia.....soma habari kamili na matukio360...#share

Na mashirika ya kimataifa

MCHEZAJI wa zamani wa soka wa kimataifa, George Weah ameshinda uchaguzi wa urais nchini Liberia na kuwa rais wa 25 wa nchi hiyo


Rais mteule wa Liberia, George Weah
Weah ambaye aliwahi kuwa mchezaji bora wa soka Duniani, amemshinda aliyekuwa makamo wa rais wa nchi hiyo Joseph Boakai.
Matokeo hayo yametangazwa leo mchana na tume ya taifa ya nchi hiyo kwa kushinda vituo 12 kati ya 15 vya kupigia kura. Takribani watu million mbili walijiandikisha kupigia kura katika uchaguzi huo wa marudio.

"Nifuraha kwa familia yangu, rafiki na wadau wangu wote walioshirikiana nami bega kwa bega kufanikisha ushindi huu wa kihistoria, sinto waangusha," amesema Weah.

Anachukua nafasi hiyo kutoka kwa rais wa kwanza mwanamke na mshindi wa tuzo ya Nobel, Ellen Johnson Sirleaf (79)

Weah (51) alishinda duru ya kwanza ya uchaguzi wa mwezi Oktoba lakini hakufanikiwa kupata asilimia 50 ya kura kumwezesha kuwa mshindi.


Duru ya pili ya uchaguzi wa urais ilichelewa kufuatia kesi iliyokuwa mahakamani.

Jana vituo vya kupigia kura vilifunguliwa saa mbili asubuhi na kufungwa saa kumi na mbili jioni.

Weah alikuwa na matumaini ya kushinda baada ya kuwania kwa mara ya tatu.

Alimshinda Bi Johnson Sirleaf wakati wa duru ya kwanza mwaka 2005, lakini akashindwa wakati wa duru ya pili.

Wakati wa uchaguzi ulioafuata akiwa mgombea mwenza, muungano wake ulisusia duru ya pili ukidai kuwepo udanganyifu.

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search