Magufuli atoa rambirambi kifo Joel Bendera...soma habari kamili na matukio360...#share
Rais John Magufuli ametuma salamu za rambirabi kufuatia kifo cha aliyekuwa mkuu wa mkoa wa Manyara Dk. Joel Nkaya Bendera kilichotokea jioni ya leo katika hospitsli ya Taifa Muhimbili (NMH) alipokuwa akipatiwa matibabu.
"Jioni hii nimepokea kwa mshtuko na huzuni kubwa taarifa za kifo cha mkuu wa mkoa mstaafu Dk. Joel Nkaya Bendera, natoa pole kwa familia yake na wote walioguswa na msiba huu na pia naungana nao katika kipindi hiki cha majonzi," amesema Rais Magufuli.





No comments:
Post a Comment