Makamu wa rais Samia Suluhu rasmi Dodoma...soma habari kamili na matukio360..#share
Na mwandishi wetu, Dodoma
MAKAMU wa rais, Samia Suluhu
kesho Desemba 15, 2017 anatarajiwa kuamia rasmi mjini Dodoma.
Makamu wa rais, Samia Suluhu
Akizunguma jana alipokuwa
akifungua mradi wa nyumba za makazi za Iyumbu Dodoma, rais John Magufuli
amesema kesho Desemba 15, 2017 makamu wa
rais ataamia mkoani humo.
Hiyo inamaana shughuli za
kiutendaji za kila siku za ofisi za makamu wa rais zitakuwa mjini Dodoma.
‘’Desemba 15, 2017 makamu wa
rais atahamia rasmi Dodoma, na mimi rais nitahamia Dodoma mwaka 2018,’’ amesema
rais Magufuli
Tayari waziri mkuu, Kassim
Majaliwa ameshahamia mkoani humo na hiyo
ni muendelezo wa watumishi wa serikali kuamia mkoani humo.
Tangu alipochukua madaraka
ya urais, Magufuli aliahidi serikali yake kuhamia mkoani Dodoma ambako ndiko
makao makuu ya nchi kutoka jijini Dar es salaam.
Sawa! Lakini mbona Mugufuli ni mkatili dhidi ya wapinzani wake! Kwa nini wachukia Rais wa Kenya Uhuru Muigai Kenyatta!
ReplyDelete