Mapinduzi Cup: Simba vs Azam, Yanga na Singida United...soma habari kamili na matukio360..#share
Na Mwajuma Juma, Zanzibar
KAMATI ya michuano ya kombe la mapinduzi imetangaza
ratiba ya michuano hiyo, huku Azam na Simba zikiwa katika kundi moja, Yanga
ikiwa na Singida United.
Kikosi cha Yanga
Michuano hiyo itakayotimua vumbi Desemba 29, 2017, itashirikisha timu 11 huku
kundi A likiwa na timu za Azam, Simba,
URA, Jamhuri na Mwenge .
Kundi B kuna timu sita ambazo ni Zimamoto, Mlandege, Taifa
ya Jang’ombe, Yanga, JKU na Singida United.
Akizungumza na waandishi wa habari katibu msaidizi wa kamati
hiyo, Khamis Shaali amesema kwa mujibu wa
ratiba hiyo siku ya kwanza ya michuano hiyo
mechi tatu zitachezwa kuanzia majira
ya saa 8;00 mchana. Mchezo wa ufunguzi ni kati ya Singida United na Mlandege.
Saa 10:00 itafuatia mechi kati ya Zimamoto na Taifa ya
Jang’ombe na saa 2:00 usiku Simba atakwaana uso kwa uso na URA.
No comments:
Post a Comment