Maulid Mtulia kugombea tena ubunge Kinondoni...soma habari kamili na matukio360...#share
Na mwandishi wetu, Dar es salaam
ALIYEKUWA mbunge wa Kinondoni kwa CUF, Maulid Mtulia ametangaza nia ya kugombea kiti hicho kupitia CCM.
Leo katika ukurasa wake wa Facebook na amelithibitishia matukio360 kuwa ni maandishi yake, ameandika:
Kwaza, nawasalimu wote na khasa wananchi wenzangu wa jimbo la Kinondoni.
Maulid Mtulia aliyeshika maiki ya akizungumza
Pili, nawapa pole sana kwa maumivu makali mliyoyapata kutokana na uamuzi wangu wa kujiuzulu ubunge wa jimbo letu la Kinondoni kupitia chama cha CUF.
Tatu, nawahakikishia kwamba bado nawapenda sana na niko tayari kuwatumikia tena kwa lengo la kuleta Maendeleo kwenye jimbo letu.
Hivyo basi, nichukie fursa hii kutangaza nia kwa wanakinondoni wote na watanzania kwa ujumla kuwa nitachukua form ya kuomba ridhaa kwenye chama changu cha CCM na endapo chama changu kitaridhia basi nitakuja mbele yenu kuomba ridhaa ya kuwatumikia katika nafasi ya ubunge wa jimbo letu Kinondoni.
Mimi mtumishi wenu,
Maulid Mtulia.
No comments:
Post a Comment