ACT Wazalendo: Hatuungi mkono mgombea yeyote ubunge, udiwani...soma habari kamili na matukio360...#share
Na Abraham Ntambara, Dar es Salaam
CHAMA cha ACT-Wazalendo kimesema hakitaunga mkono mgombea wa chama
chochote katika uchaguzi mdogo wa ubunge na udiwani unaotarajiwa kufanyika
Februari 17, 2018.
Wakwanza Kulia ni Katibu wa Itikadi na Uenezi wa ACT-Wazalendo Addo Shaibu akizungumza na waandishi wa habari hawapo pichani na wakwanza kulia ni Naibu Katibu mkuu wa chama hicho Bara Msafiri Mtemelwa.
“Kusimama na kuunga mkono mgombea wa chama fulani ni sawa na
kuunga mkono ukiukwaji wa taratibu za uchaguzi unaofanywa na NEC na vyombo vya
dola, kwa hiyo msimamo wetu hatutajihusisha kwa namna yoyote ile,” amesema
Shaibu.
Shaibu amesema kuwa wangetamani
wagombea wa vyama vya upinzani washinde lakini wanaamini kwa jinsi hali ilivyo
hawatashinda katika uchaguzi huu.
Amebainisha kuwa chama kitaungana na
vyama vingine vya upinzani katika kupigania masuala ya kidemokrasia tu na si
kwenye kusimamisha wagombea.
Awali Naibu Katibu Mkuu Bara wa chama
hicho Msafiri Mtemelwa akitoa msimamo wa chama mbele ya waandishi wa habari juu
ya ushiriki katika uchaguzi wa marudio katika majimbo ya Siha na Kinondoni amesema hakitashiriki.
“Tunapenda kuweka bayana kwamba chama
chetu hakitoshiriki kwenye uchaguzi wa marudio wa Februari 17, 2018 kwenye jimbo la Kinondoi na Siha na udiwani kwenye kata tisa,” amesema Mtemelwa.
Amefafanua kuwa msimamo huo unatokana
na ukweli kwamba sababu zilizolalamikiwa kwenye uchaguzi wa Januari 13,
2018 hazijabadilika kwa sehemu kubwa.
Amemeleza mageuzi madogo yaliyofanywa
na Tume ni kauli yao ya kuwataka wakuu wa wilaya kuacha kuingilia uchaguzi
jambo ambalo ni dogo katika malalamiko ya vyama vya upinzani.
Mtemelwa amesema chama kimeona kuna
umuhimu kwa vyama vya upinzani kuendelea kuikabili NEC na vyombo vya dola kwa
pamoja na kwaba kitaendelea kushinikiza mabadiliko muhimu kutokea ili chaguzi
ziwe huru na haki.
Pia amesema kitaendelea kushirikiana
na vyama vya upinzani na wadau wengine
wa kidemokrasia kwenye mikakati ya kushinikiza Tume na serikali kufanya mageuzi
ya mchakato wa uchaguzi.
Vyama vikuu vilivyosimamisha wagombea
katika majimbo mawili ya Siha na Kinondoni ni CCM, CUF ya Lipumba na Chadema kwa mwamvuli
wa Ukawa.
Kinondoni Wagombea ni Maulid Mtulia
(CCM), Rajab Juma (CUF Lipumba), Salum Mwalimu (Chadema) na Siha wagombea ni Elvis
Christopher Mosi (Chadema), Dk. Godwin Mollel (CCM).
Kwa mujibu wa Ofisa habari wa CUF upande
wa Profesa Ibrahim Lipumba, Abdul Kambaya akizungumza na matukio360 amesema
hadi sasa hawajapewa jina la mgombea katika jimbo la Siha hivyo wanasubiri
watumiwe ndipo watakapoliweka hadharani.
No comments:
Post a Comment