Ni George Weah au Joseph Boakai huko Liberia?...soma habari kamili na matukio360..#share
Na mashirika ya kimataifa
NCHINI Liberia, leo wananchi
wanapiga kura katika duru ya pili ya kumchagua rais wa nchi hiyo kati ya makamu
wa rais, Joseph Boakai na nyota wa zamani wa kandanda, George Weah.
George Weah kushoto na Joseph Boakai
Weah mwenye umri wa miaka 51,
alishinda duru ya kwanza lakini hakufanikiwa kupata asilimia 50 ya kura
kumwezesha kuwa mshindi.
Duru ya pili ya uchaguzi wa
urais imechelewa kufanyika kufuatia kesi
iliyokuwa mahakamani.
Vituo vya kupigia kura vimefunguliwa
saa mbili asubuhi na vitafungwa saa kumi na mbili jioni. Zaidi ya watu milioni
mbili wamejiandikisha kama wapiga kura.
Boakai mwenye umri wa miaka 73,
amekuwa makamu wa rais nchini Liberia kwa miaka 12 lakini haonekani kunufaika
na uungwaji mkono kutoka kwa rais Ellen Johnson Sirleaf,.
Naye Weah, ambaye ni nyota
wa zamani wa kandanda ana matumaini ya kushinnda baada ya kuwania kwa mara ya
tatu.
Alimshinda Hellen Johnson Sirleaf wakati wa duru ya
kwanza mwaka 2005, lakini akashindwa wakati wa duru ya pili kufuatia chama
chake kususia duru hiyo ikidai kuwapo kwa udanganyifu.
No comments:
Post a Comment