Nyumba ya rais yachomwa moto...soma habari kamili na matukio360..#share
Na mashirika ya kimataifa
MAKAZI ya rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Joseph
Kabila yamechomwa na kuteketea usiku wa kuamkia Jumatatu Desemba 25, 2017 na askari mmoja amefariki.
Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Joseph Kabila
Inasadikiwa kundi la Mai-Mai limehusika na lilitaka kuiba mali
katika nyumba hiyo iliyopo Kivu Kaskazini katika mkoa wa Bukavu.
Afisa mmoja wa jeshi amesema; "Makazi ya rais yaliyopo
Musienene yalivamiwa majira ya saa tisa usiku na kuchomwa na kundi la Mai-Mai.
Waliiba vitu kabla ya kuchoma nyumba na magari yaliyokuwapo.’’
Rais Kabila anaishi katika jiji la Kinshasa lakini anamakazi
binafsi katika maeneo mbalimbali ya nchi hiyo ikiwamo mashamba.
Kwa sasa anakabiliwa na shinikizo la kutakiwa kuondoka
madarakani kufuatia muda wake wa urais kikatiba kumalizika Desemba 2016.
Tarehe ya uchaguzi imepangwa kuwa ni Desemba 23, 2018 na kwamba uenda Kabila anataka kugombea tena. Awali ilitangazwa kuwa
ungefanyika mwaka huu(2017)
No comments:
Post a Comment